Jakaya Kikwete ni nguli na mwamba wa historia wa Tanzania na Afrika

Jakaya Kikwete ni nguli na mwamba wa historia wa Tanzania na Afrika

Uvivu wa kufanya utafiti kwani mambo yote haya lazima yatakuwemo kwenye ARCHIVES za nchi!!! Hao vijana wake wanaomuandikia speech wanayatoa wapi kwani?
Waliosoma nae wanasema alipokuwa hapo UDSM akisomea uchumi alikuwa kiazi sana!!!
Udsm nacho chuo?
Ni utumbo gani unafundishwa udsm?
 
Kikwete alikuwa Raisi Bora sana na aliruhusu Demokrasia kustawi Chini ya Utawala wake.
obama.png
 
Mashambulio dhidi ya Tanzania kutoka kwa Makabulu yamefanywa mengi tu, kuna kipindi walishawahi kushambulia sehemu za Dar es salaam kutoka baharini. Mara nyingine walijificha kwenye mabehewa ya treni inayoingia Tanzania ili wafanye yao.

Kuna mtandao wa Kijasusi ulikuwa unaitwa THE SAFARI CLUB, uliundwa na mashirika ya kijasusi ya Uajemi, Misri, Moroko, Saudi Arabia, Ufaransa, Afrika Kusini, Marekani na Israeli. Hawa ndiyo walikuwa wanafanya hujuma dhidi ya Afrika kwa kutumia migongo ya waafrika wengine kama RENAMO, UNITA, KENYA na ZAIRE.
 
Subiri akifa ndo watu wataanza unafiki.Naomba kahawa na karanga mbichi hapa ukweni
 
Kuna vitu mtu lazima ukubali kuna watu wamebarikiwa tu, Jakaya Kikwete ni mchumi lakini akisimama kwenye mimbari kuongea historia ya nchi hii wapi tumetoka, Tupo wapi na tunaelekea wapi huwezi kuchoka kumsikiliza.

Hotuba ya Jakaya Kikwete kwenye mazishi ya Nelson Mandela hakika yalifungua macho ya wengi sana kuwa JK ni mtu wa aina gani.

kilichonifanya niandike huu uzi ni hotuba yake ya juzi chuo kikuu cha Dar es Salaam kuhusu SADC imetoka wapi na ipo wapi na inaelekea wapi.

Jakaya Kikwete amesimulia kuhusu SADC mambo ambayo hata vitabuni huwezi kuvipata na ukiyapata huwezi kuyaelewa kama anavyoyafafanua kikwete kwa ustadi mkubwa sana.

Historia ya Kituo cha Polisi Salender Bridge kwa mujibu wa Jakaya Kikwete kilijengwa baada ya Makomando Makaburu wa Afrika ya kusini kutaka kulipua daraja la salender Bridge, JK anasema hao Makomando waliingia vipi na walipita wapi hakuna aliyejua mpaka pale walipoamua kusimulia wenyewe kwa kuandika kitabu, Baada ya kutega mabomu kwenye daraja la salender Bridge makaburi waliondoka kurudi kwao wakisubiri litalipuka lakini Kwa bahati nzuri daraja halikuharibika.

Baada ya Makomando Makaburu wa Afrika kusini kulikosa kosa daraja ndio Serikali ikaamua kubadilisha ile nyumba pale ya ghorofa kuwa kituo cha Polisi, Lakini kabla ya hapo pale kituo cha Polisi Salender Bridge lile jengo lilikuwa hoteli.

JK anasema Makaburu walikuwa wanatoa onyo kwa nchi zote ambazo zilikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru kusini mwa Afrika, Nchi kama Angola na Msumbiji ziliwahi kuzimiwa umeme na Makaburu kama onyo.

Hotuba ya JK kwenye msiba wa hayati Ben Mkapa kuhusu Uchumi wa kata tumetoka wapi na ni mambo gani Mkapa aliyafanya kujenga Taasisi huwezi kuchoka kusikiliza, Kikwete alisababisha watu wapate hasira baada ya ile hotuba yake pale Masasi hasa kundi la Mwendazake, Kundi la mwendazake waliona historia inaonyesha mwendazake embe dodo la Uchumi wa kati lilimuangukia tu, Lakini kazi kubwa ilifanyika awali.

Hotuba ya Kikwete kwenye Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuwa hoja haipigwi nyundo bali hujibiwa kwa hoja, Alifafanua kauli hii akieleza jinsi mwalimu Nyerere alivyokuwa anasikiliza hoja kwa umakini bila hasira wala kuchukia, Lakini kundi la Mwendazake kama Ally Hapi alikurupuka kujibu hotuba ya JK akidhani ile hotuba ilimlenga mwendazake kumbe ililenga historia ya nchi.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom