Jakaya Kikwete weka mipaka kwenye urafiki

nitajieni nchi moja duniani ambayo mtoto wa Rais ni kapuku aka rofa aka masikini...

Wakiwa matajiri tunapiga kelele, wakiwa viongozi tunapiga kelele..sasa tunatakaje jamani kama sio roho za umasikini hizi....

Watoto wa maRais au viongozi nao ni binadamu wanaohitaji kuishi kama wengine tunavyoishi, kama kuna mahala kuna opportunity nao wanahitaji kuzitumia pia...kama kuna mahala...

Baba yako akiwa Rais huruhusiwi kuwa Waziri, RC au Tajiri ?....
 
Huyo ni fisadi kama baba yake tu!! Unahangaika sana kumsafisha Huyu nyadundo!
Achana na uchawa fanya kazi ufisadi wa hiyo familia sio siri kwa WaTanzania.
 
Acha waongee tu kiongozi kelele haziwezi kuisha dunia hii kwenye ulaji lazima kuwe na maneno
Watu haohao wakipata nafasi hata kwenye ki micro credit utashangaa wanavyowekana kiundugu
 
Nani kakutuma umsemee? Umekosa kabisa la kufanya hata kulala basi
 
My friend, no need to INSULT OUR INTELLIGENCE. We’re not that stupid! Wewe huwezi kumzidi akili JK. Anajua anachofanya. Anajua anavyosuka mitandao inayomletea utajiri mchafu bila kuiathiri familia yake. Anawaendekeza Nape na January akiwaacha watoto wake? That’s really dumb.

Kama bado unapata tabu jinsi fortunes za Nape na January zilivyogeuzwa baada ya kudhalilishwa na Magufuli awamu ya 5, that’s tough. Kubali tu kuwa hao “vijana” ndio kwanza wamekabidhiwa hatamu kupindua legasi na kuneemesha wenye nchi yao. Kumsifu JK na familia yake na kuwaponda kina Nape is completely illogical and PETTY!

Sisi wananchi tunahuzunika sana jinsi CCM inavyoendelea kutufanya mazuzu na kufuja rasilimali za nchi kupitia kleptocracy, patronage, nepotism, sycophancy na outright tyranny! Hao kina JK, mwendazake na team zao ndiyo kansa kubwa kwenye maendeleo ya taifa hili. Tumeweka matumaini kwenye katiba mpya ingawa tunajua itakuwa vita kali sana kufikia marekebisho ya kweli ya mifumo ya nchi hii.
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka.
 
"Mtoa posti unaanza kuuaminisha umma mapema asubuhi kabisa ukiwa na maana unatuandaa tusije kushangaa hongera zako umeshaeleweka"
Eti anamponda Baba kisha anamfagilia Mwana !! Duh !! Inji hii alisemaga Mrema Lyatonga Wapo watu wanaishi kama wapo Peponi na wapo wengine wanaishi kama wapo Motoni !!! Tusubiri tuone what is coming next kama tutajaaliwa uhai !! Anatuandaa kisaikolojia !! Au vipi ??

Jakaya Kikwete hadi mungu afanye yake atawatesa watanzania sana​

Duh!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…