MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Wasalamu wana JF,
Wakati tukimaliza matanga ya bibi yetu Elizabeth, nimetafakari sana mienendo ya viongozi wetu hapa Tanzania. Hakika, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na madhaifu yake ni mtu mwenye hekima nyingi.
Huyu mzee alitufumbua kuhusu kuchanganya akili za kuambiwa na za kwetu. Hali kadhalika alituasa tunapoenda sehemu kwa minajili ya kuwa viongozi basi tusirithi maadui wa watangulizi wetu.
Hekima ya huyu mzee iko praticlal na mengi aliyo yasema au anayo yasema yana mafunzo makubwa, japo wengi wetu tunamchukulia poa. Kwangu mimi video hii hapa chini ni moja ya maneno yake yanayonitafakarisha sana.
"Siyo kwamba sisikii, wala siyo kwamba siambiwi yanayosemwa, au sijui kusema, au sina la kusema, la hasha! Sijafanya hivyo kwasababu sioni faida yake."
Tuendelee kumuenzi mzee wetu huyu, na Mungu amjaalie maisha marefu.