Jalada au jina la Mwesiga liliingia vipi ofisi hii takatifu?

Jalada au jina la Mwesiga liliingia vipi ofisi hii takatifu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Kuna Jambo halipo sawa ofisi ya Mhe. Rais. Kwanza huyu kwa cv yake alipataje kuwa DSO? Na Kama Mwesiga jalada lake limeingia ikulu Hadi likafika mikononi kwa Mhe. Rais Kama moja ya mtu anayefaa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara, Naibu katibu Mkuu au mkuu wa moja ya taasisi zilizopata viongozi wapya jana nataka niseme haya Kama maoni yangu;
1. Ikulu hakuna Watumishi wa Umma wenye sifa yakufanya kazi ya Ikulu hasa vetting
2. Katibu Mkuu kiongozi aliyepo ajapata muda wakutekeleza majukumu yake au hakushirikishwa
3. Viongozi wa CCM wamekalia viti vya Ikulu na wanaweka mtandao wa wizi, Kwanini apelekwe TPDC kwenye mabilioni?
4. Lipo kundi linalotaka kumwonyesha mteuaji kwamba mtanguliz was best, hawa watamwangusha wakijidai bahati mbaya
5. Msigwa pamoja na uzoefu wake si mshauri mzuri, hata jina la Kidata limekosewa
6. wanaopaswa kumshauri Rais wanaogopa kufanya hivyo, wazee waliondolewa
7. Mama anafanyia kazi mapendekezo ya Bashiru na JPM
8. Watu wanamchomekea.

Nini kifanyike?
Uteuzi uanzie kwa Katibu Mkuu Kiongozi, majina yatakayopita yaambatanishwe na CV. Kama wanataka kuteua kada Basi waweke utaratibu makada wote waweke cv kwenye file za chama Kama tunaogopa kufukua taarifa za mtu kwakumtaka awasilishe. Tuachane na vijana wa system maana hawana uwezo tuteue kulingana na uzoefu unaoonekana.

Kwa sababu;
Kwa cv ile nadhani waliohusika kupeleka jina lake walifanikiwa maana haya Mambo yameruhusiwa kufanywa na kikundi Cha watu bila formal procedure. Kwa Sasa waliohusika wanapaswa kuadhibiwa ili huu mchezo usiendelee Tena wakuchomekea watu wasiofaa kuwa viongozi.
 
Katika majina yooote , moja ndo limeonekana Lina shida , lakini lawama Kwa mama zimekuwa nyingi ..... Na bado kalifanyia kazi , yeye siyo Mungu bhana ..... Tafuteni watoto wenu hela ya Kula
 
Wa atz manenoo mengiiiiiiiiiiiiiii (in bba Kesca voice)

Mwacheni mama apige kazi acheni viherehere kujifanya mnajua watu kumbe zeroo (in baba jesca voice)
 
Kwa mtazamo wangu vetting committee iangaliwe upya....utumishi wa umma una watu wengi Sana wenye sifa.Kipindi Cha jpm Kuna watu waliingizwa kwenye nafasi za teuzi wasio na sifa za utumishi
 
Kwa mtazamo wangu vetting committee iangaliwe upya....utumishi wa umma una watu wengi Sana wenye sifa.Kipindi Cha jpm Kuna watu waliingizwa kwenye nafasi za teuzi wasio na sifa za utumishi
Hiyo committee ipo sasa ? majina yanatoka lumumba na Tiss
 
Katika majina yooote , moja ndo limeonekana Lina shida , lakini lawama Kwa mama zimekuwa nyingi ..... Na bado kalifanyia kazi , yeye siyo Mungu bhana ..... Tafuteni watoto wenu hela ya Kula
Kuna siku tukiwa primary kuna mtihani nilipata 92%, na bado nikachapwa na mwalimu wa somo bakora nyingi kuliko hata waliopata 20%. Hasira za mwalimu, ni kwanini nimekosa swali rahisi, na lilikuwa rahisi kweli.

Anyways, kuna mambo matatu makubwa hapa
1. Umuhimu wa hili shirika
2. Sifa za mtu anayeondoka
3. Sifa za huyu anayekuja.

Nina uhakika kuna watu watapoteza nafasi zao kwa sababu ya hili saga. Kwamba jamaa hakufaa kuwekwa hapo, lilikuwa ni jambo rahisi mno kung'amua. Personally nilihisi kuna mtu amekosea kuchapisha taarifa.
 
Hao ndio wanabeba mafaili nyeti ya nchi kwahiyo kunyofoa jina na kujipachika wao ni kawaida sana
Hakuna vetting wala mavi ya vetting, itafika siku house girl wangu anateuliwa kuwa RC sitashangaa
 
Mimi ningekua presda nisinge mtumbua kesho yake asubuhi.. nimemsubilisha hata baada ya mwezi mmoja au miwili lakini asingekanyaga ofisini angekuwa mkurugenzi jina tu.

Hii ingelinda heshima ya aliyeteua na aliyeteuliwa. Lakini kumfukuza few hours baada ya uteuzi ni weakness kubwa kwa mteuaji kwamba anateua watu asiowajua
 
Nimejaribu kuona watu wanahoji....huyu Mwesiga alikuwa DSO Kigoma, Makamu anatokea Kigoma. Je haiwezekani akawa alisaidia kitu huko Kigoma analipwa fadhilila? Lakini Kama ni fadhila ndo apewe nafasi kubwa kiasi hicho? Lakini Kama Mkurugenzi wa TPDC anaweza akapatikana kizembe hivi, wakuu wa wilaya, wakuu wa vyombo na wakurugenzi wa halmashauri si watu wataza ndugu zao?

Ila pia huko ikulu na huko kwenye vetting TISS Kuna Wazalendo na watu wenye wivu na Tanzania? Je, viongozi wa dola Kama wanashindwa kulinda ajira hizi nyeti wanaweza kulinda ajira zao na waliochini yao zisipokwe na politicians? Kwann tunaruhusu watu kupata nafasi kizembe hivi? Lini senior official waserikali wataongoza taasisi zao walizokulia?
 
Karibia asilimia 97 ya hizi teuzi ni watu wamebadilishiwa vituo vya kazi tu, ila ni wale wale.
Katika majina yooote , moja ndo limeonekana Lina shida , lakini lawama Kwa mama zimekuwa nyingi ..... Na bado kalifanyia kazi , yeye siyo Mungu bhana ..... Tafuteni watoto wenu hela ya Kula
 
Nimejiuliza sana pia jina liliingiaje Ikulu?
 
Na kwa hayo tu uliyoorodhesha inaonekana watu wanaweza kuichezea IKULU watakavyo. Kama Ikulu inaweza kuchezewa hivyo ambayo ndio ofisi muhimu kuliko ofisi ya kwanza kuliko ofisi yoyote Tanzania,je vipi ofisi ambazo ni ndogo,wanaweza kupeleka vitanda ofisini kama Lipumba.

Hapo si kuondoa makada Ikulu ila hata anayewekwa Ikulu na wananchi naye inabidi atolewe na wananchi ili ofisi za aina hiyo zisafishwe. Maana kwa Tanzania Chama ni kikubwa kuliko nchi.
 
Swali hapa ni kuwa huyu mmoja tulimgundua haraka Sana tukapiga kelele Mama akatengeua..

Je ambao hatujawagundua na wanaenda kuapishwa kesho??..


Na je hii team yake iliyopeleka jina lake imepeleka mangapi?Na kama yamepita wanajiandaa na dili zipi?
 
Ikulu iliharibika siku nyingi. Tangu enzi za MWinyi watu kwenda Ikulu na mifuko ya 'rambo.' JPM ndo aliyeanza kuirudisha kwenye sifa yake na ndo wa kwanza kuwaondoa waliochomekwa dk. za mwisho. Kumbukeni wakati wa kuapisha wakurugenzi 2016.

Kuna kundi linatoa sifa nyiingi kwa Samia lakini lengo ni moja, lionekane na kurudishwa madarakani. wapo vijana kibao waliovurunda. Akina Kigwangala, Nape, Januari, naona na mzee Kinana yumo na tweets za sifa! Dah! Wanataka kurudi!!!!!!!!!!
 
Si wangechomeka kwenye nafasi ya DAS au RAS lakini sio shirika lenye dhamani ya mabilioni tena nyeti kabisa.
 
Karibia asilimia 97 ya hizi teuzi ni watu wamebadilishiwa vituo vya kazi tu, ila ni wale wale.
Wengi wao walifanya chini ya kiwango. Ila nina mashaka sana kuna watu wana agenda binafsi ktk timu ya washauri wa Rais ni kama wanataka ashindwe.

Kuna watu wengi sana ktk wale makatibu wakuu ni hovyo sana. Na yupo mmoja ni mpya ninamfahamu uwezo wake anaenda ktk wizara ambayo mama alitoa muda iundwe ndani ya miezi 3. He's typical academia na aliwahi kuwa DG NSSF muda mfupi kabla ya kutolewa, pale palihitaji mtu mzoefu aliyewahi kuwa katibu mkuu awali.
 
Back
Top Bottom