Jali afya yako - Yajue maajabu ya mwili wako

Jali afya yako - Yajue maajabu ya mwili wako

Mtafiti1

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2011
Posts
263
Reaction score
148
Unaweza ukashangaa kujua kwamba:
1. ULIMI wako ni kama alama zako za vidole! Ukitaka usitambuliwe basi ficha huo ulimi wako maana unaweza kutumika kukubamba kama unatafutwa kama vile finger prints zinavyotumika.

2. Ngozi yako inajivuka kama nyoka anavyovua gamba!Kila saa magamba 600,000 mithili ya mba hupukutika! Usishangae unapooga ukajifuta utaona taulo linachafuka hapohapo! Kila mwaka utatoa kiasi cha magamba/mba wenye uzito wa kilo moja kwa mwaka!

3. Idadi ya mifupa ya mtu mzima ni ndogo kuliko ya mtoto mchanga. Mtoto huzaliwa na mifupa 350 na anapokuwa, hii mifupa huunganika hadi kubaki mifupa 206.Usishangae sana unapoona mtoto akiwa flexible zaidi ya mtu mzima.

4. Tumbo lako nalo lina maajabu. Ulijua kuwa tumbo lako linapata lining mpya kila siku 3-4 kwa vile acid/vimeng'enya vya chakula humeng'enya tumbo lako pia.Ulishawahi kutapika sakafuni ( siyo juu tiles au udongo) ukaona jinsi acid ya tumboni ilivyo kali? Isingekuwa kubadilisha lining basi tumbo lako lingetoboka!

5.Utumbo mdogo/mwembamba una urefu mara nne ya urefu wa wastani wa mtu mzima.Unakadiriwa kuwa na urefu wa futi 18 hadi 23! Isingekuwa kwamba umesokotwasokotwa kwa namna ya ajabu , usingeenea tumboni.

6. Bacteria walio juu ya ngozi yako ni wengi hadi idadi inatisha! Hutaamini kwamba kila inchi ya mraba ya ngozi ya mwili ina bacteria wapatao milioni 32! Usiogope kwa maana wengi hawana madhara kwako.

7.Harufu mbaya katika maeneo mbalimbali ya mwili wako kama makwapa, miguu n.k inatokana na jasho.Miguu peke yake ina uwezo wa kutoa karibu nusu lita ya jasho kwa maana ina glendi za jasho zipatazo 500,000!

8. Damu yako husafiri umbali mrefu sana kila siku!Ingewezekana kupanga mishipa yako kmithili ya barabara, basi ingefikia urefu wa maili 60,000, na kila siku moyo ulio na afya hu husukuma lita 7571 kila siku.Halafu tukiambiwa tuchunge afya ya moyo kwa kula vyakula visvyo na mafuta ili kuepusha lehemu kuganda ndani ya mishipa, au kuishi maisha yasiyo na stress zisizo na lazima, hatuzingatii kivile.Tujue pump hii ( moyo) haina spea! ikiharibika mchezo ndio unaishia hapo. Punguza kunywa pombe, kuvuta sigara; fanya mazoezi ya kutosha ili kuuweka moyo katika afya.

9.Mate tunayotoa kwa siku, ingewezekana kuyakusanya basi ingetosha kujaza mabwawa mawili ya kuogelea kwa maana yanafikia lita 23,700!

10.Uzito wa kichwa cha mwanadamu ni robo ya uzito wake anapozaliwa na ndio maana watoto wanashindwa kukaza vichwa vyao wakiwa wachanga.Uliza mama aliyekwishakua na mtoto atakuambia kwamba lazima ukimbeba umshikilie shingo kisogoni kukibalance!Tunapofikai utu uzima, uzito wa kichwa ni 1/8 ya uzito wa mwili.
 
Na mguu wa tatu unatema kiasi gani?
 
Mavuzi jee? Kila mwaka ni kilo ngapi?
 
Kweli Mungu katuumba kwa maajabu. Miili yetu ni very complex!
 
Duu!. Asante kuna mengi hatukuyajua. Kwa kuongezea.
1. Mwili wa binadamu unapojiumiza, kujikata, kidonda, kuchubuka etc, hujitibu wenyewe bila dawa yoyote. Nyingi za dawa za vidondo sio kuleta uponyaji bali kuzuia maambukizi ya bacteria.
2. Kwenye upasiaji kazi ya kushonwa na nyuzi ni ili kuweka mgandamizo tuu na sio kuunganisha, mwili hujiunganisha wenyewe!.
3. Mfupa wa binadamu ukivunjika hujiunganisha wenyewe bila kuungwanishwa na chochote. Hata zile POP hazina tiba yoyote bali kuusaidia mfupa usijipinde tuu.
4. Kwa kutumia mazoezi maalum ya meditation, mwili wa binadamu una uwezo wa kuona visivyoonekana na kusikia visivyosemwa ikiwemo kusoma mawazo ya mtu.
5. Mwili wa binadamu una uwezo wa kufanya chochote kupitia "will Power" hivyo hata hiyo miujiza watu wanaofanyiwa muujiza husika hufanywa na mwili wa mhusika na sio yule mhubiri.
 
Back
Top Bottom