Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Mwanamke anataka ajisikie unamjali.
Yaani unajali hisia zake za upendo kwako. Ila drama zake unaweza kupotezea.
Utamuonesha kujali hisia zake kwa kutenga muda kwa ajili yenu. Mkatengeneza kumbukumbu mbali mbali kwa kwenda sehemu tofauti au kucheza pamoja na kufurahi pamoja. Na kumpa mapenzi motomoto.
Hivyo vitamfanya ajisikie salama kwako, kiuchumi, kiroho, kimwili na kihisia. Naye atakujali zaidi.
Kama usipomzingatia hisia zake. Au ukamfanya ajisikie vibaya kwa kukuonesha hisia zake ataona humjali. Na atajitoa kwako.
Mpaka muda huo hatojali wewe ni mzuri kiasi gani, au una hela kiasi gani, au ni mtu wa watu kiasi gani, au mmeishi pamoja kwa muda gani. Kwake ataangalia anajisikiaje kuhusu wewe anapokufikiria.
Chochote anachojisikia akikufikiria ndicho ataamini atajisikia akiwa nawe.
Hivyo, akijisikia vizuri akikufikiria atataka kuwa nawe zaidi.
Mahusiano yatakua rahisi na mtaishi kwa furaha.
Lakini kama unamuudhi kila saa, unamnyenyekea mno au haumfanyi ajisikie hamu na wewe hatotaka muonane. Ndo hapo ataanza kukuzungusha au kukuchunia kabisa.
Kumjali mwanamke sio kumuweka juu yako, au kumuona ndo kila kitu na inabidi umfurahishe na usimkosee, kumtukuza/ kumnyenyekea, kubadili ratiba/ bajeti zako ili kumuonesha unampenda. Bali ni kumfanya ajisikie amani kujiachia kwako na kujiachia hisia zake kwako kwa kuwa jasiri kumuongoza vile utakavyo.
Nikutakie Weekend Njema na Maandalizi Mema Ya Wiki Ijayo. Pia Uwe na Sikukuu Njema yenye Amani.