Jamaa ajizolea umaarufu mitandaoni kwa kuamua kukisubiria kimbunga Milton katika boti yake huko Florida USA

Jamaa ajizolea umaarufu mitandaoni kwa kuamua kukisubiria kimbunga Milton katika boti yake huko Florida USA

State Propaganda

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2024
Posts
542
Reaction score
1,286
Joseph Malinowski almaarufu kama 'Lieutenant Dan' amejikuta akitrend toka jana katika mitandao ya kijamii haswa Tik tok na X baada ya kukataa kuondoshwa katika kijiboti chake na askari polisi ili kupelekwa sehemu salama kufuatia ujio wa kimbunga hatari cha Milton (category 5), kinachotarajiwa kutia nanga leo Oktoba 10 katika pwani ya Florida. Kimbunga Miltkinafananishwa na kimbunga Helene kilichoipiga pwani ya Florida juma moja tu lililopita.

Kutokana na madhara makubwa nayayotegemewa kutokea huko jimboni Florida, imebidi askari polisi kutaka kutumia nguvu Kumto mzee huyo, ambaye aliweka ngumu kutoka katika kijiboti chake. Baada ya kuona jamaa hataki kutoka, mwishowe polisi waliamua kuanza kumbembeleza na kumfariji Lieutenant Dan huku wakiwa nje ya boti yake

Wakati Dan akizidi kutrend, kampuni moja ya michezo ya kubashiri ikaamua kutumia fursa hiyo ambapo bets kama ata savaive ama la zimewekwa huku watu wakitupia vibunda kujaribu bahati zao.

IMG_20241010_142151.jpg
IMG_20241010_142353.jpg
Screenshot_2024-10-10-14-22-26-88.png
 

Attachments

  • IMG_20241010_142123.jpg
    IMG_20241010_142123.jpg
    153.2 KB · Views: 8
Je hizo kampuni zitamlipa au ndio wanatumia TU nafasi yake kujineemesha!?binafsi nashauri akomae kimbunga kikipita adai hela.
Yeye mwenyewe kama anaona ata survive inatakiwa aweke mzigo.

Pakitokea ubishi mahala fulani halafu ajitokeze mtu aseme mimi naonfoa ubishi juu ya jambo fulani wekeni hela zenu. Unadhani mtu huyo anawajibika kulipia hilo jambo?
 
Nachoweza kusema ni R. I. P Lieutenant Dan maana kimbunga cha category 5 kama Milton ni zaidi ya malaika mtoa roho.
View attachment 3120945
kwenye radar ya ndege ikionyesha hivyo af rubani akaforce kupita hapo kati ., kitakachotokea ni kwamba ndege +waliomo ndani wanagawanyishwa vipisi kama mtu aliyekanyaga pakti ya biskuti.
 
Hivi kwa wenzetu mtu kuchoronga mwili ni jambo la kawaida eeh! Maana naona wengi sana wamejichorachora wakati kwetu huku hiyo ni dalili mbaya na uhuni
 
Back
Top Bottom