Jamaa ajizolea umaarufu mitandaoni kwa kuamua kukisubiria kimbunga Milton katika boti yake huko Florida USA

Jamaa ajizolea umaarufu mitandaoni kwa kuamua kukisubiria kimbunga Milton katika boti yake huko Florida USA

Joseph Malinowski almaarufu kama 'Lieutenant Dan' amejikuta akitrend toka jana katika mitandao ya kijamii haswa Tik tok na X baada ya kukataa kuondoshwa katika kijiboti chake na askari polisi ili kupelekwa sehemu salama kufuatia ujio wa kimbunga hatari cha Milton (category 5), kinachotarajiwa kutia nanga leo Oktoba 10 katika pwani ya Florida. Kimbunga Miltkinafananishwa na kimbunga Helene kilichoipiga pwani ya Florida juma moja tu lililopita.

Kutokana na madhara makubwa nayayotegemewa kutokea huko jimboni Florida, imebidi askari polisi kutaka kutumia nguvu Kumto mzee huyo, ambaye aliweka ngumu kutoka katika kijiboti chake. Baada ya kuona jamaa hataki kutoka, mwishowe polisi waliamua kuanza kumbembeleza na kumfariji Lieutenant Dan huku wakiwa nje ya boti yake

Wakati Dan akizidi kutrend, kampuni moja ya michezo ya kubashiri ikaamua kutumia fursa hiyo ambapo bets kama ata savaive ama la zimewekwa huku watu wakitupia vibunda kujaribu bahati zao.

View attachment 3120932View attachment 3120933View attachment 3120934
Hatima yake ilikuaje? Tupe feedback
 
Hivi kwa wenzetu mtu kuchoronga mwili ni jambo la kawaida eeh! Maana naona wengi sana wamejichorachora wakati kwetu huku hiyo ni dalili mbaya na uhuni
Huku hupati kazi Govt....au vyombo ulinzi
 
Back
Top Bottom