Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

The Masterpiece

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
562
Reaction score
1,544
Wakuu habari zenu,
Mwaka jana mwezi March kuna jamaa mtaani hapa aliniibia kuku mchana kweupe kabisa watu wanaona, nilipopata taarifa nikamtafuta mtaani nikamkosa, nikaamua kwenda nyumbani kwako nikamkuta dada zake nikawaeleza jamani fulani kaniibia kuku wangu naomba akija mwambieni arudishe. Hawakutilia sana maanani wakasema wamechoka na habari zake za wizi ila watamwambia arudishe.

Niliporudi mtaani nikapata taarifa kutoka kwa wambea wa mtaa ya sehemu alipouza hao kuku ikabidi nifunge safari mpaka kwa huyo mama aliyeuziwa kuku lakini nae akakataa kabisa kuwa hajauziwa. Basi me nikaondoka, kesho yake mchana nikapewa taarifa kuwa mwizi wangu ameonekana mtaani huko eti ananitafuta ajue kwa nini namchafulia jina lake mtaani, ikabidi sasa nianze kumtafuta hali ya kuwa kichwani tayari nimechafukwa kwa hasira. Muda si mrefu nikakutana nae kabla sijaongea nae akaanza kunipandishia sauti kwa nini nimeenda kwao nimemuita mwizi wa kuku, hapo uzalendo ukanishinda kwa hasira nikavaana nae nikampiga kidogo then nikamchukua nikampeleka mpaka ofisi ya mtaa kushtaki kuwa mwizi wangu huyu naomba anirudishie kuku wangu.

Alipoulizwa kuhusu kuiba kuku akakataa kabisa tena akaniruka kuwa nimempiga sana hali ya kuwa kuku hajaiba, me kuulizwa ushahidi sina zaidi ya kutaka kwenda alipouza kuku, tukaongozana mimi, mwizi wangu pamoja na mtendaji wa mtaa mpaka alipouza kuku, kufika hapo aliyenunua kuku akakataa kabisa kuwa hajauziwa kuku. Hapo nikakosa ushahidi wa kumtia hatiani ikabidi niwe mpole tu ila nikatamka kuwa basi namuachia Mungu kama kweli hajaiba kuku na iwe hivyo lakini kama ameiba basi Mungu atalipa kwa wote waliohusika, nikaondoka zangu.

Sasa ikapita miezi kama sita tukio limeanza kusahaulika, akaja jirani mmoja kunipa habari kuwa yule mwizi wangu anaumwa sana na anaropoka huko usiku wa manane kuwa kuku wamemponza, sikutilia maanani sana habari hizo maana najua umbea wa mtaani labda walitaka kunichimba wajue kama nikisamehe kweli au kuna kitu nilifanya. Baada ya kama wiki mbili hivi habari zikaenea zaidi kuwa jamaa anaumwa sana na amewaambia ndugu zake kuwa anakufa kwa sababu ya kuku. Baada ya siku kadhaa akaja mzee mmoja ni sheikh wa msikiti ninaosali hapo mtaani akaniambia kuwa amefuatwa na familia ya mwizi wangu kuwa yeye sheikh ameitwa kumuombea dua mgonjwa ambaye ndio huyo mwizi wangu, baada ya dua familia imemtuma aje kwangu kuomba msamaha kwa niaba yako maana hali imekuwa ngumu sana. Me nikamjibu sheikh "mzee wangu mimi sihusiki kabisa na ugonjwa wa huyo mtu, tangu nilipokosa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu kuku wangu aliowaiba basi nikasamehe kwa maana kwanza kuku wenyewe hawakuwa wengi lakini pia nikiendelea kufuatilia hii issue nitapoteza muda lakini pia nitajijengea ubaya na ndugu zake kwa hiyo nimesamehe kwa roho moja"
Mzee anaondoka.

Sasa leo alfajir nikiwa msikitini ndio nikasikia tangazo la kifo cha jamaa aliyeniibia kuku wangu, kibinadamu niliingia huzuni lakini nikahisi sasa watu wamepata cha kusema kuhusu Mimi na huyu jamaa, wakuu tangu muda huo story mtaani ni mimi kuhusika na kifo cha jamaa, wengine wanasema sawa tu jamaa alizidi, wengine wanasema Nina roho mbaya yaani kuku tu ndio natoka roho ya mtu. Basi sina amani na hata msibani kuzika nafikiria nisihudhurie maana hata wasionijua watatambulishwa leo kuwa mimi ndio muhusika.

Cha kushangaza yule mama niliyeambiwa kuwa ndio alinunua kuku niliobiwa, asubuhi kanifuata nyumbani eti kuniomba msamaha, kakiri ni kweli aliuziwa kuku wangu na yule jamaa na sio kuku wangu tu hata kuku wa watu wengine pia huwa anamuuzia na mbuzi alishawahi kununua kwa jamaa. Nikamjibu kuku wangu mimi ni wale weupe akasema ndio aliwanunua ila anaomba msamaha yuko tayari kulipa pesa ya hap kuku ila nisifanye kitu kibaya katika familia yake au yeye maana anajua tego la mwizi huwa linaanza na mwizi, aliyenunua mpaka aliyekula hivyo ana hofu familia yake itaangamia. Nikamjibu mama we kuwa na amani mimi sihusiki na hilo. Ameondoka lakini hana raha kabisa.

Wakuu nakiri mbele yenu nyinyi sijawahi hata kuusogelea ushirikina na sihusiki kabisa na hili lakini ndio hivyo nimeshapata sifa mbaya mtaani, naombeni ushauri wenu katika hali hii nifanye nini angalau niwe na amani.

Shukran.
 
Kuna mtu wa karibu ameamua kukusaidia kazi kijana,the thing ni kuwa huyo jamaa alikuwa anaiba sehemu nyingi kuku mtaani kwa hiyo unatakiwa ufahamu ya kwamba sio wewe peke yako uliyewahi kuibiwa kuku kitaa,kwa hyo Kuna mtu katika circle yenu mlioibiwa kaamua kusafisha mtaa.vinginevyo iwe ni wachawi wa mtaani kwenu kwa kuwa wanafahamu uhasama wenu .Impact ya jambo Hilo ni kuwa ndugu zake watataka kukumaliza wewe,siku sio nyingi utarogwa na ndugu zake au na wachawi wa mtaani kwenu.kama ni wachawi wa kitaa the next round inakuhusu wewe kufa ili ionekane kuwa kisasi kimelipwa na ndugu.wachawi Huwa wanatumia akili kubwa sana kwenye mambo yao ndugu,usione furaha huyo mtu kufa .Hakuna mtu ataiba Tena kitu nyumbani kwako ila fahamu kuwa haupo salama wewe na familia yako.mara nyingi watu wa pwani hata kama watoto wao Wana makosa hawawezi kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa.Hapo jambo la msingi unatakiwa kuhama.Vinginevyo mama aliyenunua kuku anahisi kufa tuu wakati wowote ,kwa hiyo lazima ahakikishe anakutanguliza ili awe safi.kama unarafiki yako wa karibu anayefanya fanya ibada mara tano kwa siku na ulimweleza jambo Hilo fahamu kuwa aliamua kukulipia kisasi kimya kimya.
 
Unaogopa nini Sasa ? Jiamini Sasa tegemea kuheshimika Sana mtaani ,ndiyo muda wa kupandisha mabega na kiwapiga biti wakikuletea ujinga
 
Kuna mtu wa karibu ameamua kukusaidia kazi kijana,the thing ni kuwa huyo jamaa alikuwa anaiba sehemu nyingi kuku mtaani kwa hiyo unatakiwa ufahamu ya kwamba sio wewe peke yako uliyewahi kuibiwa kuku kitaa,kwa hyo Kuna mtu katika circle yenu mlioibiwa kaamua kusafisha mtaa.vinginevyo iwe ni wachawi wa mtaani kwenu kwa kuwa wanafahamu uhasama wenu .Impact ya jambo Hilo ni kuwa ndugu zake watataka kukumaliza wewe,siku sio nyingi utarogwa na ndugu zake au na wachawi wa mtaani kwenu.kama ni wachawi wa kitaa the next round inakuhusu wewe kufa ili ionekane kuwa kisasi kimelipwa na ndugu.wachawi Huwa wanatumia akili kubwa sana kwenye mambo yao ndugu,usione furaha huyo mtu kufa .Hakuna mtu ataiba Tena kitu nyumbani kwako ila fahamu kuwa haupo salama wewe na familia yako.mara nyingi watu wa pwani hata kama watoto wao Wana makosa hawawezi kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa.Hapo jambo la msingi unatakiwa kuhama.Vinginevyo mama aliyenunua kuku anahisi kufa tuu wakati wowote ,kwa hiyo lazima ahakikishe anakutanguliza ili awe safi.kama unarafiki yako wa karibu anayefanya fanya ibada mara tano kwa siku na ulimweleza jambo Hilo fahamu kuwa aliamua kukulipia kisasi kimya kimya.
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana ambacho nami kinaniumiza kichwa, je baada ya msiba ndugu zake watakubali tu yaishe hali ya kuwa wanahisi me ndio nimemroga ndugu yao? Je wakisema walipe kisasi wanidhuru si itakuwa dakika 0 tu maana sijui mambo ya kishirikina kabisa. Akili nyingine inaniambia nitafute wataalam wanikinge sasa si ndio itakuwa najiingiza kwenye maagano ya kichawi?
 
Back
Top Bottom