Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

Itakuwa nafsi yako nyingine imemuadhibu. Wengine huwa wana nguvu. Kidini wanasema malaika mlinzi wako. So your guardian angel amefanya yake kulipa kisasi baada ya wewe kusema unamwachia Mungu. Usipoangalia hata huyo mama aliyenunua kuku anaenda kupigwa
 
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana ambacho nami kinaniumiza kichwa, je baada ya msiba ndugu zake watakubali tu yaishe hali ya kuwa wanahisi me ndio nimemroga ndugu yao? Je wakisema walipe kisasi wanidhuru si itakuwa dakika 0 tu maana sijui mambo ya kishirikina kabisa. Akili nyingine inaniambia nitafute wataalam wanikinge sasa si ndio itakuwa najiingiza kwenye maagano ya kichawi?
Usijali, kilicholipiza kisasi ni walinzi wako. Hawawezi kukubali uguswe. Wana nguvu sana. Trust me
 
Wakuu habari zenu,
Mwaka jana mwezi March kuna jamaa mtaani hapa aliniibia kuku mchana kweupe kabisa watu wanaona, nilipopata taarifa nikamtafuta mtaani nikamkosa, nikaamua kwenda nyumbani kwako nikamkuta dada zake nikawaeleza jamani fulani kaniibia kuku wangu naomba akija mwambieni arudishe. Hawakutilia sana maanani wakasema wamechoka na habari zake za wizi ila watamwambia arudishe.

Niliporudi mtaani nikapata taarifa kutoka kwa wambea wa mtaa ya sehemu alipouza hao kuku ikabidi nifunge safari mpaka kwa huyo mama aliyeuziwa kuku lakini nae akakataa kabisa kuwa hajauziwa. Basi me nikaondoka, kesho yake mchana nikapewa taarifa kuwa mwizi wangu ameonekana mtaani huko eti ananitafuta ajue kwa nini namchafulia jina lake mtaani, ikabidi sasa nianze kumtafuta hali ya kuwa kichwani tayari nimechafukwa kwa hasira. Muda si mrefu nikakutana nae kabla sijaongea nae akaanza kunipandishia sauti kwa nini nimeenda kwao nimemuita mwizi wa kuku, hapo uzalendo ukanishinda kwa hasira nikavaana nae nikampiga kidogo then nikamchukua nikampeleka mpaka ofisi ya mtaa kushtaki kuwa mwizi wangu huyu naomba anirudishie kuku wangu.

Alipoulizwa kuhusu kuiba kuku akakataa kabisa tena akaniruka kuwa nimempiga sana hali ya kuwa kuku hajaiba, me kuulizwa ushahidi sina zaidi ya kutaka kwenda alipouza kuku, tukaongozana mimi, mwizi wangu pamoja na mtendaji wa mtaa mpaka alipouza kuku, kufika hapo aliyenunua kuku akakataa kabisa kuwa hajauziwa kuku. Hapo nikakosa ushahidi wa kumtia hatiani ikabidi niwe mpole tu ila nikatamka kuwa basi namuachia Mungu kama kweli hajaiba kuku na iwe hivyo lakini kama ameiba basi Mungu atalipa kwa wote waliohusika, nikaondoka zangu.

Sasa ikapita miezi kama sita tukio limeanza kusahaulika, akaja jirani mmoja kunipa habari kuwa yule mwizi wangu anaumwa sana na anaropoka huko usiku wa manane kuwa kuku wamemponza, sikutilia maanani sana habari hizo maana najua umbea wa mtaani labda walitaka kunichimba wajue kama nikisamehe kweli au kuna kitu nilifanya. Baada ya kama wiki mbili hivi habari zikaenea zaidi kuwa jamaa anaumwa sana na amewaambia ndugu zake kuwa anakufa kwa sababu ya kuku. Baada ya siku kadhaa akaja mzee mmoja ni sheikh wa msikiti ninaosali hapo mtaani akaniambia kuwa amefuatwa na familia ya mwizi wangu kuwa yeye sheikh ameitwa kumuombea dua mgonjwa ambaye ndio huyo mwizi wangu, baada ya dua familia imemtuma aje kwangu kuomba msamaha kwa niaba yako maana hali imekuwa ngumu sana. Me nikamjibu sheikh "mzee wangu mimi sihusiki kabisa na ugonjwa wa huyo mtu, tangu nilipokosa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu kuku wangu aliowaiba basi nikasamehe kwa maana kwanza kuku wenyewe hawakuwa wengi lakini pia nikiendelea kufuatilia hii issue nitapoteza muda lakini pia nitajijengea ubaya na ndugu zake kwa hiyo nimesamehe kwa roho moja"
Mzee anaondoka.

Sasa leo alfajir nikiwa msikitini ndio nikasikia tangazo la kifo cha jamaa aliyeniibia kuku wangu, kibinadamu niliingia huzuni lakini nikahisi sasa watu wamepata cha kusema kuhusu Mimi na huyu jamaa, wakuu tangu muda huo story mtaani ni mimi kuhusika na kifo cha jamaa, wengine wanasema sawa tu jamaa alizidi, wengine wanasema Nina roho mbaya yaani kuku tu ndio natoka roho ya mtu. Basi sina amani na hata msibani kuzika nafikiria nisihudhurie maana hata wasionijua watatambulishwa leo kuwa mimi ndio muhusika.

Cha kushangaza yule mama niliyeambiwa kuwa ndio alinunua kuku niliobiwa, asubuhi kanifuata nyumbani eti kuniomba msamaha, kakiri ni kweli aliuziwa kuku wangu na yule jamaa na sio kuku wangu tu hata kuku wa watu wengine pia huwa anamuuzia na mbuzi alishawahi kununua kwa jamaa. Nikamjibu kuku wangu mimi ni wale weupe akasema ndio aliwanunua ila anaomba msamaha yuko tayari kulipa pesa ya hap kuku ila nisifanye kitu kibaya katika familia yake au yeye maana anajua tego la mwizi huwa linaanza na mwizi, aliyenunua mpaka aliyekula hivyo ana hofu familia yake itaangamia. Nikamjibu mama we kuwa na amani mimi sihusiki na hilo. Ameondoka lakini hana raha kabisa.

Wakuu nakiri mbele yenu nyinyi sijawahi hata kuusogelea ushirikina na sihusiki kabisa na hili lakini ndio hivyo nimeshapata sifa mbaya mtaani, naombeni ushauri wenu katika hali hii nifanye nini angalau niwe na amani.

Shukran.
Ntume Muhammad (SAW) anasema , watu watatu Dua zao hazirejeshwi ( zinakubaliwa moja kwa moja) . Wa kwanza Kiongozi muadilifu , wa pili Aliyefunga mpaka afuruturu na Maangamizo ya aliyezulumiwa .Sasa hapo ndo pamemuondosha uyo jamaa .
 
Mkuu hilo tayari limeshakujengea heshima mtaani.
Hata ukiacha hela nje ya nyumba hakuna atakayezigusa.
Kwa kuwa hukumdhuru kwa lo lote endelea na maisha yako.
 
Nipatie namba ya mganga wako tafadhali
 
Ulishamuachia Mungu.Mungu ndie anaejua kama anatekeleza ulichomuachia au anatimiza wajibu wake.
Ila mwizi siyo kumuonea huruma
 
Mambo ya kwa msisi, handeni, Tanga
 
Acha woga hakuna mtu atakudhuru.
Huwezi kuzuia hisia na maneno ya watu.
 
Nimeshuhudia matukio mawili ya watu kufa, sababu ya kuku,...mmoja aliiba kuku vizuri kabisa,sasa wakati anakimbia akaingia kwenye shimo lililochimbwa kwa ajili ya kupanda mgomba, akavunjika mgongo, akakutwa asubuhi akiwa mzima, ila watu wakagoma kumsaidia mpaka akafa , maana walisema alikuwa msumbufu sana, na huwezi amini alikuwa na wake wawili,.....

wengine ilikuwa pale mbeya karibu na shule ya iyunga boys, walienda kuiba kuku, jirani wa mwenye kuku alikuwa katoka kupiga masanga akawaona wakiwa wanatoboa ukuta, akawashtua wengine kwa simu, wezi wakajaa kwenye kumi na nane... wawili wakala kiberiti,..mmoja tu ndo alipokonyoka,......

Kuku..🙌🙌🙌
Kwamba hta wake zake walishindwa kuja kumsaidia
 
Hapo ndo vizuri unatakiwa uvimbe ili wajinga wajinga waache kukuzoea kitaani, watakuwa wanakuita MZEE WA BUSARA 😹

Na msibani usiende achana nao waache wazike mwizi wao..!!!
Hapo wewe fungua kilinge upige pesa za wajinga sasa.!! Chuma majani ya muarobaini yakaushe kazi ianze, si umesema msikitini huwa unaenda enda so kiarabu unakijua cha kunywea maji?? 😹

Wapandishie majini ya uongo na kweli, watume wakuletee kuku ukazie zile zilizoibiwa..!!
 
Wakuu habari zenu,
Mwaka jana mwezi March kuna jamaa mtaani hapa aliniibia kuku mchana kweupe kabisa watu wanaona, nilipopata taarifa nikamtafuta mtaani nikamkosa, nikaamua kwenda nyumbani kwako nikamkuta dada zake nikawaeleza jamani fulani kaniibia kuku wangu naomba akija mwambieni arudishe. Hawakutilia sana maanani wakasema wamechoka na habari zake za wizi ila watamwambia arudishe.

Niliporudi mtaani nikapata taarifa kutoka kwa wambea wa mtaa ya sehemu alipouza hao kuku ikabidi nifunge safari mpaka kwa huyo mama aliyeuziwa kuku lakini nae akakataa kabisa kuwa hajauziwa. Basi me nikaondoka, kesho yake mchana nikapewa taarifa kuwa mwizi wangu ameonekana mtaani huko eti ananitafuta ajue kwa nini namchafulia jina lake mtaani, ikabidi sasa nianze kumtafuta hali ya kuwa kichwani tayari nimechafukwa kwa hasira. Muda si mrefu nikakutana nae kabla sijaongea nae akaanza kunipandishia sauti kwa nini nimeenda kwao nimemuita mwizi wa kuku, hapo uzalendo ukanishinda kwa hasira nikavaana nae nikampiga kidogo then nikamchukua nikampeleka mpaka ofisi ya mtaa kushtaki kuwa mwizi wangu huyu naomba anirudishie kuku wangu.

Alipoulizwa kuhusu kuiba kuku akakataa kabisa tena akaniruka kuwa nimempiga sana hali ya kuwa kuku hajaiba, me kuulizwa ushahidi sina zaidi ya kutaka kwenda alipouza kuku, tukaongozana mimi, mwizi wangu pamoja na mtendaji wa mtaa mpaka alipouza kuku, kufika hapo aliyenunua kuku akakataa kabisa kuwa hajauziwa kuku. Hapo nikakosa ushahidi wa kumtia hatiani ikabidi niwe mpole tu ila nikatamka kuwa basi namuachia Mungu kama kweli hajaiba kuku na iwe hivyo lakini kama ameiba basi Mungu atalipa kwa wote waliohusika, nikaondoka zangu.

Sasa ikapita miezi kama sita tukio limeanza kusahaulika, akaja jirani mmoja kunipa habari kuwa yule mwizi wangu anaumwa sana na anaropoka huko usiku wa manane kuwa kuku wamemponza, sikutilia maanani sana habari hizo maana najua umbea wa mtaani labda walitaka kunichimba wajue kama nikisamehe kweli au kuna kitu nilifanya. Baada ya kama wiki mbili hivi habari zikaenea zaidi kuwa jamaa anaumwa sana na amewaambia ndugu zake kuwa anakufa kwa sababu ya kuku. Baada ya siku kadhaa akaja mzee mmoja ni sheikh wa msikiti ninaosali hapo mtaani akaniambia kuwa amefuatwa na familia ya mwizi wangu kuwa yeye sheikh ameitwa kumuombea dua mgonjwa ambaye ndio huyo mwizi wangu, baada ya dua familia imemtuma aje kwangu kuomba msamaha kwa niaba yako maana hali imekuwa ngumu sana. Me nikamjibu sheikh "mzee wangu mimi sihusiki kabisa na ugonjwa wa huyo mtu, tangu nilipokosa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu kuku wangu aliowaiba basi nikasamehe kwa maana kwanza kuku wenyewe hawakuwa wengi lakini pia nikiendelea kufuatilia hii issue nitapoteza muda lakini pia nitajijengea ubaya na ndugu zake kwa hiyo nimesamehe kwa roho moja"
Mzee anaondoka.

Sasa leo alfajir nikiwa msikitini ndio nikasikia tangazo la kifo cha jamaa aliyeniibia kuku wangu, kibinadamu niliingia huzuni lakini nikahisi sasa watu wamepata cha kusema kuhusu Mimi na huyu jamaa, wakuu tangu muda huo story mtaani ni mimi kuhusika na kifo cha jamaa, wengine wanasema sawa tu jamaa alizidi, wengine wanasema Nina roho mbaya yaani kuku tu ndio natoka roho ya mtu. Basi sina amani na hata msibani kuzika nafikiria nisihudhurie maana hata wasionijua watatambulishwa leo kuwa mimi ndio muhusika.

Cha kushangaza yule mama niliyeambiwa kuwa ndio alinunua kuku niliobiwa, asubuhi kanifuata nyumbani eti kuniomba msamaha, kakiri ni kweli aliuziwa kuku wangu na yule jamaa na sio kuku wangu tu hata kuku wa watu wengine pia huwa anamuuzia na mbuzi alishawahi kununua kwa jamaa. Nikamjibu kuku wangu mimi ni wale weupe akasema ndio aliwanunua ila anaomba msamaha yuko tayari kulipa pesa ya hap kuku ila nisifanye kitu kibaya katika familia yake au yeye maana anajua tego la mwizi huwa linaanza na mwizi, aliyenunua mpaka aliyekula hivyo ana hofu familia yake itaangamia. Nikamjibu mama we kuwa na amani mimi sihusiki na hilo. Ameondoka lakini hana raha kabisa.

Wakuu nakiri mbele yenu nyinyi sijawahi hata kuusogelea ushirikina na sihusiki kabisa na hili lakini ndio hivyo nimeshapata sifa mbaya mtaani, naombeni ushauri wenu katika hali hii nifanye nini angalau niwe na amani.

Shukran.
Shusha na huyo mnunuzi wa mali za wizi udongoni.

Madalali na wanunuzi wa mali za wizi ndo chanzo cha uhalifu mwingi mtaani
 
Kama ni mwizi basi kuna mtaalam mmoja aliiba kwake akaamua amle kichwa.
Kama hujahusika huna haja ya kuwaza. Kama una mawazo sana, Hama huo mtaa uwe huru. Usije kufa kwa stress
 
Nimeshuhudia matukio mawili ya watu kufa, sababu ya kuku,...mmoja aliiba kuku vizuri kabisa,sasa wakati anakimbia akaingia kwenye shimo lililochimbwa kwa ajili ya kupanda mgomba, akavunjika mgongo, akakutwa asubuhi akiwa mzima, ila watu wakagoma kumsaidia mpaka akafa , maana walisema alikuwa msumbufu sana, na huwezi amini alikuwa na wake wawili,.....

wengine ilikuwa pale mbeya karibu na shule ya iyunga boys, walienda kuiba kuku, jirani wa mwenye kuku alikuwa katoka kupiga masanga akawaona wakiwa wanatoboa ukuta, akawashtua wengine kwa simu, wezi wakajaa kwenye kumi na nane... wawili wakala kiberiti,..mmoja tu ndo alipokonyoka,......

Kuku..[emoji119][emoji119][emoji119]
Binadamu wakikuchoka ni hatari, jamaa wa shimoni akakosa msaada
 
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana ambacho nami kinaniumiza kichwa, je baada ya msiba ndugu zake watakubali tu yaishe hali ya kuwa wanahisi me ndio nimemroga ndugu yao? Je wakisema walipe kisasi wanidhuru si itakuwa dakika 0 tu maana sijui mambo ya kishirikina kabisa. Akili nyingine inaniambia nitafute wataalam wanikinge sasa si ndio itakuwa najiingiza kwenye maagano ya kichawi?
Hakuanga kisasi katika shikri kinachofanya kazi kama wewe hujahusika mkuu! Nilichokiona kwako ni hofu kuwa vipi kama ndugu wa familia wakiamua kukufanyia na wewe shirki kama malipizi.

Laana isiyo na sababu haimpati mtu! ... Kuwa na amani ... Kuwa mtu wa ibada! Unawezaje kuwa unamtegemea Mungu na kumwabudu then uogopa wachawi? This mean Mungu wako unamuona Hana nguvu na huamini kuwa anaweza kukulinda dhidi ya ushirikina.

Usirihusu hofu kukutawala maana hofu ndio mlango mkubwa sana ambao adui anaweza kuutumia kukumaliza.

Kile walichohofia na kukiogopa ndicho kilichowapata ... Siku zote hofu Ina adhabu.

Usikubali hofu
 
Hii Kuna jamaa alisota mahabusu Kwa miaka 3,yeye alienda kutishia bibi kizee mchawi wa mtaani kuwa atampiga mapanga akiendelea kumroga,,,issue ya vitisho vya jamaa ilienda viral mtaani sasa Kuna miamba ambayo ilisharogwa kitambo na huyo bibi ikatumia fursa ya vitisho vya jamaa kumaliza kazi Kwa kumkata kata panga bibi kizee,,, suspect wa kwanza aliye toa vitisho na alisota mahabusu miaka Hadi kutoka,,,hata wewe kinachokugharimu ni vitisho vyako Kwa huyo marehemu mwizi.

Cha kufanya jikinge vizuri maana next move ni kurogwa pia na ndugu za marehemu.
 
Back
Top Bottom