Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

Kuna meme inasomeka BONGO MTU ANAKWAMBIA NAMUACHIA MUNGU KISHA ANAKWENDA KUKUROGA.

Nenda msibani, shirikiana nao vizuri wafiwa kwa kila linalofaa kushirikiana, tulia kimya, usianzishe stori yoyote kuhusu jambo hilo, yeyote atakayekuface kwa hoja hiyo mwambie ittaqillaah, (mche/muogope mola) majibu yako yawe mafupi mafupi, anayekuomba radhi mwambie hujanikosea kitu nk
 
Ila wachawi lazima waku test,sema watagundua huna kitu wataachana na wewe!
Ndugu zake si walikujibu wamemchoka na habari za wizi,sidhani kama wataangaika na wewe.
Ila Kuna mwamba kafanya kazi hio...Linda Sana ulimi na reaction zako kwenye jamii.
 
Ama kweli ukifa mke wako asiolewe
 
Soma Uzi wa The dark side of business hapa JF ,mleta mada anakwambia kabisa njia ya mafanikio ni the light side haijalishi wanadamu watakuonaje au watakusemaje mtangulize Mungu kwa hakika hili nalo litapita
 
Ukihisiwa hivyo ndio vizuri mkuu. Umejenga jina. Raia watakuwa hawakuibii kibwege.
 
Mi kuna mmoja namlia Timing. Yeye naye wamechoka hapa mtaani. Yule ameniibia sana. Sasa nimeleta kuku za nyama nafuga hapa kwangu na nimefunga camera shambani.

Sasa akiniibia nimepanga nimgonge na gari nimvunje miguu yake tu. Hao ni wapumbavu sana.
 
Ulivyosema unamwachia Mungu ulitarajia nini?Umehusika aise.Ungejua ungesamehe tu.
 
Hakuna kitu kina mikosi mikubwa kama kuku....
Niliibiwa pikipiki nikiwa kazini....kesho yake nikaambiwa aliyeiba hiyo pikipiki kagongwa na gari nakufa hapo hapo! Miaka sita Baadaye...niliibiwa TV, nguo na viatu na wezi wawili...baada ya Mwaka Mwizi mmoja kauwawa kwa risAsi walipoenda kufanya ujambazi mwingine miezi Saba baadaye inasemekana amepoteza hajulikani alipo! Bahati mbaya sana sikuwahi kukutanishwa nao au kuwajua kwa sura wezi hawa!!!

Nilivyokuwa nikibiwa Sara yangu ilikuwa ni kumuomba Mungu tukio hili walilolifanya kwangu liwe tukio lakuwafanya wabadili tabia zao na kuwa raia wema.
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…