Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

Mkuu mimi sijamtisha jamaa zaidi ya kumwambia basi nimesamehe namuachia Mungu na hiyo ilikuja baada ya kukosa ushahidi wa dhati wa kumpeleka polisi pia niliona ingenipotezea muda kwa kitu kidogo kama kuku tu.
 
Yeye ni mwizi, ameiba kuku sehemu mbalimbali. Alivyokuwa akitaja kuku wamemponza, ina maana kuna sehemu kaiba kuku kawekewa tego ila kwa kuwa wewe uligombana naye laivu ndio maana wanahisi ni wewe.

Hii ni mbaya sana mana watu wanaweza kukuogopa na hata familia yake wanaweza kulipa kisasi.

Mtu akikuuliza, mwambie siyo wewe inawezekana ametegewa sehem nyingine mana alikuwa mwizi wa kuku aluyekububu
 
We tulia tu. Hudhuria mazishi ili watu wakutambue. Hakuna mtu atadokoa kitu chochote kwako mpaka ufe. Mungu amekutengenezea kinga. Zidi kumwomba Mungu, ndivyo anavyowafanyia waovu. Kuwalipizia kisasi wanaonewa.
 
Jiepusheni na tupu mbili.
1.mdomo
2.uke au ume
maangamio ya wengi yanatokana na moja kati ya vitu hvyo viwili.

NB:Kilichokuponza ni mdomo, cha kufanya kaa kimya muda utakusaidia kuongea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…