Jamaa anaitwa Mohamed ameibiwa watoto 2 saa 12 jioni na mfanyakazi wa ndani Wilaya ya Temeke

Jamaa anaitwa Mohamed ameibiwa watoto 2 saa 12 jioni na mfanyakazi wa ndani Wilaya ya Temeke

Siku hizi wadada wa kazi wanapatikana kwa agents wa huko vijijini wanwatafuta mabinti yaan kazi yako kumpa sifa za binti unayemtaka tu, unatuma nauli na posho yake afu anakutumia binti.
Hao ma agent unawaamini vipi? Ni ujinga wa kiwango cha SGR kuletewa mfanyakazi wa ndani na mtu usiyemfahamu kisa tu mnawasiliana kwenye simu
 
What if kama imezima chaji? Tunazijua vizuri simu za wafanyakaz wa ndani zinavyokuwaga? Tena ana siku 3 kutoka kijijini na mshahara usikute anamlipa elfu 30 Kwa mwezi
Umeshajua wamepatikanaje hao watoto?
 
Hao ma agent unawaamini vipi? Ni ujinga wa kiwango cha SGR kuletewa mfanyakazi wa ndani na mtu usiyemfahamu kisa tu mnawasiliana kwenye simu
Una familia? Mkeo ana majukumu ya utafutaji tofauti na kukaa nyumbani? Ni mara ngapi umekosa binti ukaenda mwenyewe kutafuta kijijini na ukampata ndani ya muda ulioupanga wewe? Yapo mambo mengi yanawafanya watu inabidi wanawaamini tu mabinti maana nao ni binadamu kama watu wengine ni basi tu inatokea tabia, malezi, yanatofautiana ila wapo mabinti wema kabisa
 
Acha tuu sasa ndio hivyo tufanyeje
Suala sio mtafanyaje Bali mnatakiwa kuwa makini hasa wanawake maana ndio wadau wakubwa, mfanyakazi wa ndani ni mtu muhimu sana unatakiwa umjue angalau background ya familia anayotokea funga hata safari nenda Kwa watu wake huyo ni mtu utakayemuavhia nyumba, watoto wako na kuchukua dhamani ya chakula pia kwahiyo kama humjui vyema basi unabet Maisha ya familia Yako.
 
Muache kulipa hawa mabinti TSH 60000/month, wakichoka utumwa huwa wanakuwa hatari sana hawa.

Kumbuka house girl anakaa na watoto wako nyumbani.
Huyo binti alikuwa na siku 2 tu ya tatu ndo akatoka na watoto akidanganya anafika nao dukani ndio kutokomea na watoto
 
Suala sio mtafanyaje Bali mnatakiwa kuwa makini hasa wanawake maana ndio wadau wakubwa, mfanyakazi wa ndani ni mtu muhimu sana unatakiwa umjue angalau background ya familia anayotokea funga hata safari nenda Kwa watu wake huyo ni mtu utakayemuavhia nyumba, watoto wako na kuchukua dhamani ya chakula pia kwahiyo kama humjui vyema basi unabet Maisha ya familia Yako.
Kumjua mtu na familia sio kuujua moyo wake na dhamira, binti unakuta umemchukua kwa wazazi wake vizuri unawajua ila tayari yeye alishajifunza mengi ya kidunia ambayo hata mama ake mzazi hajui, anashawishika anafanya majanga na kwao harudi
 
Kama familia yake na Binti mwenyewe umewafahamu vyema kamwe Binti hawez kukuletea shida otherwise uwe unamnyanyasa ktka kazi na malipo pia .
 
Tunarudi kule kule tunapowaambia kati ya kulea watoto na kazi kipi cha muhimu? sasa hivi hawalali na hawali
Wako tiyari kutoa hata m100 ili mradi watoto wapatikane wakiwa hai.Siku zote ukweli kamwe haubadiriki kulingana na mazingira eti kwa sababu maisha ni magumu ni bora kwenda kutafuta wote me/ke matokeo yake ndio haya.

Dunia ya sasa hivi siyo ya kumuamini mtu yeyote hadi kufikia level ya kumuachia familia yako watoto na mali kuanzia saa12 asubuhi hadi saa2 usiku. Ukweli sisi tunopinga tutaendelea kuonekana washamba na wakoloni kwa kuzuia wake zetu kwenda kufanya kazi. Naamini familia ni bora sana kuliko pesa inayoenda kutafutwa na mke wangu yeye abaki nyumbani na watoto ndo mlinzi pekee mwaminifu kwa familia akiongozwa na baba wa familia.

Haya matukio huwa yananikumbusha mwaka 2016 Dodoma nzuguni.Dada alipata mfanyakazi kutoka iringa pale tulikuwa na watoto2 wote wa kike.Mfanyakzi yule akaagizwa dukani kwenda kununua Tambi mida ya 11 jioni akaenda hadi saa1 haonekani.

Hofu ikaingia tukaanza jufuatilia kufika dukani akasema alinunua mbona na kurudi na alikuwa na watoto2 mmoja akiwa amembeba mgongoni. Hpo huyu binti alikuwa na wiki tu tangu aje.....saa2 tukaenda kutangaza mskitini lakini wapi tukataja na no za simu hatukufanikiwa.

By saa3 tupo kituo cha police tukaamliwa kama hatapatiakana hadi kesho turudi tena.....Muda tumewaambia wazazi kijijni simu kila dk wajukuu wetu wamepatiana dada analia tu mme wake yupo nje ya nchi nae simu kila muda ....hatukula wala kulala.Baadhi ya majirani walikuja tukawa nao hapo kama 3 hadi asbh tukaendele kutafta bila bila.

kwenye saa3 tukapigiwa simu police tuwafate ...kale kabinti kalipotea njia kaakenda hadi kwenye mji kakajieleza bahati mbaya mtaa tunaoishi binti haujui na kwa dada hamji hata jina anamueleza ni wa rangi hii na kabila lake ni ........

Tena walienda kwenye mji huo ni baada ya mtoto aliyekuwa anatembea akachoka kutembea na yeye hawezi kuwabeba woteTambi alikuwa nazo tukawabeba hadi home ndipo tukakumbuka kuwa jana hatukula wala kuoga.

Tukio hili lilinipa funzo kubwa mno japo sikuwa na mtoto lakini nilikuwa nawaza sijui kamewauza sijui wamechinjwa yaani nilikuwa nawaza mabaya tu hadi dk tunaambiwa wapo police.

NARUDIA WATOTO NA FAMILIA MUHIMU SANA KULIKO HIZO MILIONI 3 UNAZOINGIZA KILA SIKU KWENYE BIASHARA YAKO.SIKU YAKIKUTA UTAKUMBUKA MANENO HAYA.

Mungu awafanyie wepesi watoto hao wazuri wapatikane wakiwa hai na afya tele
 
Kama familia yake na Binti mwenyewe umewafahamu vyema kamwe Binti hawez kukuletea shida otherwise uwe unamnyanyasa ktka kazi na malipo pia .
Mkuu omba tu uwe unapata mabinti wema kuijua family sio sababu kabisa hapo umerahisishiwa tu sehemu ya kuanzia likitokea lolote kama hili. Sasa hivi tupo mbele ya muda sana hata mdogo wake na mke wako usimwamini kwenye watoto wako unayepaswa kumuamini ni mama zenu na mke wako tu.

Matukio haya yamekuwa mengi sana. Mimi siwezi muachia mdada wa kazi jukumu la kunilelea watoto siwezi.Niliona kapostiwa na millad ayo hapo gharama tiyari zimeanza kutoa na muda huo unakuwa njia panda kama utawapata au lah!!
 
Back
Top Bottom