Jamaa anajuta sana kwa hili,Wewe je unajutia nini?

Pacbig

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2017
Posts
1,095
Reaction score
2,087
Katika maisha kuna wakati unafanya maamuzi lakini mwisho wa siku pasipo kutarajia,Maamuzi hayo yanatoa matokeo mabaya mara nyingine ya kuumiza sana unabaki tu kujutia.

Niliwahi kupewa story na brother mmoja ambaye mama yake alikuwa mtu wa huzuni nyingi na masikitiko makubwa kwa sababu aliolewa lakini kwa bahati mbaya watoto aliowazaa walikuwa wanafariki kabla ya kutimiza mwaka mmoja, alipoteza watoto sita.Jambo lililomfanya achukiwe na ndugu na jamaa za mmewe lakini mme wake alimpenda sana hakumuacha.

Kipindi kilifika Yule mama akapata tena mimba lakini mme wake aliugua ugonjwa wa akili na siku chache waliukuta mwili wake umetupwa jalalani amefariki akiwa na majeraha haikujulikana chanzo hasa cha kifo.Mama yule aliumia sana lakini mara nyingi aliamini mtoto aliyepo tumboni hatafariki ila atakua na ataishi miaka mingi na kumrudishia angalau furaha iliyopotea ni kweli alijifungua lakini siku aliyojifungua alipoteza damu nyingi sana ukizingatia alikuwa kwenye zahanati ndogo sana hivyo kupoteza maisha siku hiyohiyo lakini mtoto alitoka mzima na akalelewa na bibi yake mzaa baba.Na ndo brother aliyenipa story.

Huyu brother alikulia maisha magumu sana,akiwa bado kijana akawa anajishughulisha na kazi za viwandani.Alikuja kupendwa msichana mrembo sana na mtoto wa kitajiri aliyempenda sana.Yule mrembo alimtambulisha kwao wazazi wakamkubari wakampa hadi pikipiki ya bodaboda ili imusaidie kiuchumi.Kuna kipindi katika maisha unapenda sana hadi unakuwa kama kichaa hasahasa kwa kijana aliyekulia maisha magumu lakini akapata mapenzi ya dhati.

Siku moja akiwa anaendesha kwa kasi sana pikipiki akiwa amembeba huyo mpenzi wake pikipiki ilipata hitilafu ikawa haipunguzi mwendo na breki zilifeli.Kwa sababu jamaa alimpenda sana Yule mwanamke akaazimia kutomuambia juu ya lile tatizo huku akimpa element avae.yule mwanamke akamuuliza kwanini, jamaa akajibu yeye anaona ni nzito.Alipomuambia apunguze mwendo akasema anajisikia raha kuendesha pikipiki kwa kasi hakutaka amwambie ukweli ili asipate presha.

Walipata ajali mbaya sana mwisho wa siku Yule jamaa akapata hitilafu kwenye ubongo akalemaa miguu na mikono.Hakuweza kufanya kazi nyingine tena akabakia ombaomba na akawa mlemavu.Yule mwanamke aliumia kidogo na alipopona akamuacha kisa hawezi kuolewa na mlemavu na ombaomba.

Jamaa kitu anachojutia zaidi kwenye maisha ni kitendo cha kumpa element mpenzi wake.Ningependa kushare na wewe kuhusu unachokijutia zaidi Kwenye maisha.
 
Nilichogundua nikwamba we nimuongo ulietukuka hakuna pkipki inayo feli brek na ikashindikana kupunguza speed inaomesha we cyo dereva mzee yani kama ni chai bac sukari haijakolea au umeichanga na chumvi mzee baba watu tunaendesha pkpk hazina hata brek lkn haiwi kama ulivyo simulia ww. Asante chai yako lakn haijakolea sukari
 
Hii ni hatari lakini kwenye maisha kuna muda unaweza ukahisi yangu makubwa lakini wapo watu hawasemi yao hayasemeki kabsa bali yanajieleza tu
 
Ndivyo nilivyosimuliwa na mhusika siwezi kubadilisha nilivyoambiwa
 
Kwahiyo moral of the story ni tusisaidie tunaowapenda kwasababu tunaweza kuja kujuta??
Unaonekana hujaelewa mimi nimelichukua kwa mjibu wa mhusika ndo anachojutia.Ndo nikaona tushee our biggest regret kwenye maisha mamb ya moral yapo out of concerns.
 
Bado sijaelewa neno la 'element' alilosaidiwa mwanamke kuvaa ni kitu gani, yaani element inavaliwa?
Kofia maalumu kwa matumizi ya kuendesha pikipiki ili kujikinga na majeraha kichwani endapo ikitokea ajali.
 
Pikipiki ipo kasi hadi anapata muda wa kuvua Helmet na kumpa mchumbake. Hii chai imekosa Mlonge.
 
Pikipiki ipo kasi hadi anapata muda wa kuvua Helmet na kumpa mchumbake. Hii chai imekosa Mlonge.
 
Safi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…