Wakuu nawasalimu.
Kitu kilichotokea kwa akina Halima Mdee siyo cha kushangaza. Ni mwendelezo wa matukio mengi tu ambayo yamekuwa kawaida siku hizi.
Watu wanaotumia muda kufikiri, wakiwemo pia ndani ya CCM wanajua kinachoendcelea. Unawezaje kuwalaumu akina Mdee? Ukitaka
kutoa lawama kwa hawa, utatakiwa pia uwalaumu makumi ya wengine, toka kwa akina Moses Machali, Julius Mtatiro, David Kafulila na wengine hadi akina David Silinde, Joshua Nassari na Vicent Mashinji na wenzao.
Ukiangalia chaguzi zote, kuanzia zile ndogo, tangu kuingia kwa Rais John Magufuli, unatambua dhamira halisi ya viongozi ni kuondoa upinzani. Hii ni awamu pekee ambayo CCM imepata ushindi mkubwa katika kila uchaguzi kuliko wakati mwingine wowote. Inapata ushindi katika nyakati ambazo wimbi la vijana, ambao ndiyo wengi kukichoka chama hicho likiwa linazidi kuwa kubwa. Kama nilivyosema pale awali, wenye kutumia angalau muda kidogo tu kufikiri, wanajua kinachotokea. Kuna mchezo mchafu unaochezwa ili haya mambo ya kuitia nchi aibu yatokee.
Lakini unajiuliza, hivi hawa wanaofanya haya mambo, huwa wanafikiria wanachokifanya? Tuangalie tu tukio hili la akina Halima Mdee, achana na wale waliotangulia kuunga mkono juhudi.
Leo serikali inapata fedheha kwa sababu tu ya wapanga mipango kukosa maono. Kinacholazimishwa hapa, ni kutengeneza bunge lenye wapinzani ili kupata uhalali wa kupokea shilingi trilioni 2 za misaaada toka nje kila mwaka.
Hivi hili hawakulitambua mapema?
Kama walilitambua, kwa nini hawakuachia majimbo angalau ya wapinzani wasioumiza ili kupata uhalali huu? Hivi hawakuona kuwa vitendo vile vya waziwazi vitawafanya wasuse? Kama wapanga mipango wangekuwa na maonoi haya, ni wazi kuwa hili jambo lisingetokea leo. Wangeweza kuwanyima Chadema jimbo hata moja, lakini wakawapa vyama vile 'rafiki' japo viti 30 vya kuzugia.
Leo hii, dunia nzima wanajua mchezo huu mchafu unaoidhalilisha ofisi ya Tume ya Uchaguzi, ofisi ya Bunge na vyombo vya uchunguzi ambavyo ni dhahiri hawatafanyia kazi tamko la Chadema kuwa barua na mchakato mzima umeghushiwa.
Ipo haja kwa CCM kuipangua kamati yake ya mipango kwa sababu imekosa weledi. Nchi hii ilipofikia CCM haina uwezo wa kushinda kwa asilimia 80. Ndiyo maana inahaha kujinasua na ulaghai huu na hivyo inazidi kufanya makosa.