Nampa pole. Kama mwanaume, alifanya kosa kubweteka kwa kukaa na kusubiri kununuliwa na kutunzwa na mwanamke. Mi maisha yangu yote sijawahi kusikia baba wa nyumbani, mara nyingi nimesikia mama wa nyumbani. Alipaswa kuomba mtaji kipindi kile ambacho huyo dada alikuwa anamhudumia ili afanye shughuli za kujitegemea.
Sishangai sana huyo dada kuamua kumpiga chini huyo kaka, maana labda ameona kuwa ni mtu asiyefikiria mambo ya maendeleo, imagine kipindi chote hicho hataki kujishughulisha, ataweza vipi kusimamamia familia yake kama akipewa nafasi ya kuwa mume?
Mshauri rafiki yako, abadili tabia. Nasita mno kumtetea.