Mbona jamaa kasema ukweli mtupu? Anafanya nini rumande?
Na Mwandishi wetu (Nipashe)
2nd September 2009
Raia wa Iraq, Anney Anney, anayedaiwa kuwakashifu viongozi, amepelekwa rumande baada ya kesi ya kuwakashifu marais wa awamu ya pili na tatu kuahirishwa tena Septemba 7 mwaka huu kutokana na upande wa mashtaka kudai upelelezi bado haujakamilika.
Kesi hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Samuel Maweda
Baada ya kesi hiyo kuahirisha, mshtakiwa huyo mwenye ulemavu wa mguu, aliiomba mahakama hiyo kumruhusu ajidhamini kwa madai kuwa tangu apelekwe gerezani amekosa mawasiliano na ndugu zake wanaotakiwa kufika kumwekea dhamana.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo Julai 27, mwaka huu na kusomewa mashtaka ya kutoa maneno ya uchochezi na kuwakashifu marasi hao kwa kuendesha nchi kwa maslahi yao binafsi.
Inadaiwa kuwa Julai 23, mwaka huu, majira ya mchana katika eneo la Ikulu jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alitoa maneno ya uchochezi kuwa Rais wa Awamu ya Pili, Hassan Mwinyi aliua Azimio la Arusha na wa tatu Benjamin Mkapa mashirika ya umma na ardhi kwa wazungu na waarabu na utu wa utaifa wa Watanzania .
Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kuwa baada ya kutamka maneno hayo alisema udumu ujamaa na kujitegemea , lidumu Azimio la Arusha na zidumu fikra za Mwalimu Nyerere.
Mshtakiwa huyo alikana shaka hilo na kupelekwa rumande baada ya mahakama hiyo kukataa ombi la kujidhamini kwa kukosa wadhamini.