Jeff Gemo
Member
- Jul 11, 2015
- 34
- 26
Salaam wana JF.
Jana kupitia kipindi cha michezo Radio Times "Wizara ya Michezo" nimesikia kwa masikio uchi kabisa bila kisaidizi namna ambavyo Malinzi anaendesha (au pengine kuendeshwa..Who knows!) Soka la nchi hii.
Kuna kesi ambayo haijajulikana inaisha lini, madai ya muda mrefu ambayo yanatakiwa kutafutiwa ufumbuzi kwa wakati. Wale Geita walikataa kutoa rushwa na ndio ukawa mwisho wao, tena wakaporomoshwa wala sio kushushwa.
Jamaa akaenda mbali zaidi kwa kuonesha nyaraka za ripoti ya ukaguzi zikionesha Bw. Malinzi kujilipa mamilioni ya shilingi bila kueleza sababu wala kuweka kiambatanisho (supporting Documents), na sio mara moja.
Ukiachana na hilo kabla kichwa hakijapoa, hawa DTB walikuwa tayari wana mabango yao uwanjani lakini jana (19/9/2016) ndio wameingia mkataba (haikuwa ku"re-new"), sasa mtu unaweza kujiuliza waliwezaje kuweka mabango bila mkataba? Na kama upo kwanini ulikuwa ni wa siri?
Usichoke, namalizia moja ya mwisho kwa leo, hii pesa yenyewe sasa ni Milioni 250 lakini nafasi waliyopewa eti kuwa Bank rasmi sijui utumbo gani.. Hivi CRDB waliishia wapi?? Wao walikuwa na shilingi ngapi?? Hii kitu TFF walitangaza wapi?? Hiyo pesa kweli kabisa unaweza kusema ni udhamini??
Achilia mbali timu za daraja la kwanza kulazimishwa kuprint nembo la mdhamini bila maslahi, mgao wa kibabe wa Azam TV na mazingaombwe mengine yote.. Ninachojiuliza ni kwamba Bwana Malinzi ana nani nyuma yake anayemkingia kifua?
Hakuna mpenzi wa michezo nchini anayemkubali Malinzi, ameshafeli muda mrefu sana na hata yeye anajua kwamba hapendwi na haungwi mkono.
Rais anashindwa mambo madogo tu kama kutweet taarifa sahihi ambazo hata wewe msomaji unaweza kufanya ukiwa usingizini, jamaa hawezi kabisa yaani lazima atoe boko hata kama yupo uwanjani. Sasa mambo makubwa yanayohitaji kutumia akili tunawezaje kumtegemea??
Sasa haya malalamiko ya Geita yenye ushahidi wa maandishi na mengine sauti inamaana hayajafika kwa vyombo husika? Sasa mbona hatusikii chochote??? Yaani mnataka kutuaminisha kwamba Malinzi haguswi?? Na yeye anajua kwamba hatoguswa ndio maana anafanya anayoyafanya?? Nani huyo anayempa kiburi???
Tangu aondoke mzee wetu Tenga kila kitu kimekuwa ovyo, soka linaporomoka na hamasa imeshuka, hakuna mtu anataka kuunga mkono mambo yasiyoeleweka, hata ligi kuu yenyewe tunajilazimisha tu kwa mahaba ya timu zetu lakini sio vinginevyo.
Wale Geita wamesema waislamu huenda kuhiji Mecca, na wakristo huenda Israel, sasa wao kama wasiposikilizwa madai yao, wamesema watakwenda kuhiji Chato mpaka kieleweke... Mimi ndio nasubiri hapo tu.
Ok, nimalize na hii homework.. Tumtafute aliye nyuma ya Malinzi, anayekwamisha hizi kesi na kudumaza soka letu, tumuulize kwa heshima, hekima, busara na upole, TULIMKOSEA NINI SISI WATANZANIA??
Jeff Gemo Mnyama Machine
The One Man Army
Affirmative Gemo The Great
[HASHTAG]#SeriesFreeLife[/HASHTAG]
Season 2 | Episode 2