Jamal Malinzi na tuhuma za udini

Jamal Malinzi na tuhuma za udini

Daah mngekuwa wanafunzi mngechezea stick vibaya. Hiyo ni lugha Ya picha alotumia Jamal Malinzi akimaanisha since hawaendi kuchagua viongozi wa dini! Maadili sio muhimu ndo maana akamchagua mla rushwa Joseph Blatter
 
Last edited by a moderator:

Boss, umeitafsiri vizuri. Ila kwenye soka pia kuna maadili, na rushwa ni adui kila mahali. Bado kauli yake haiko sawa.
 
Last edited by a moderator:
Inaonekana watu wengi wamedakia tu hiyo tweet ya Malinzi, hawaijui historia ya FIFA na hawajafuatilia matukio ya karibun yanayoihusu FIFA.

Mtangulizi wa Blatter, Joao Havelange, waweza kusema aliiweka kando Afrika na hata Asia ktk uongoz wake. FIFA ilikuwa ya ulaya na amerika kusin kwa kiasi kikubwa. Ikumbukwe, Afrika ina kura zaid ya 54 za urais wa FIFA. Blatter aliona mwanya huo na akautumia vyema na anaendelea kuutumia. Pia Blatter amekuwa kipaza sauti cha Afrika na Asia na kwingneko ambako wanachama hawana saut ndan ya FIFA. Blatter ndiye aliyeleta kombe la dunia Afrika, ndiye analeta pesa za maendeleo ya soka k mamilion. Hili wazungu weng hawapend maana mabilion ya Fifa meng yanatoka kwao. Kwanin yaende Afrika?

Kwa FIFA ya Havelange, Afrika isingenusa kombe la dunia, achilia mbal kuandaa. Blatter ndiye aliyeamua kombe la dunia liandaliwe kimabara kwa zamu, la sivyo wangekuwa wanapasiana ulaya na amerika kusin.

So ni kweli Blatter ni mzuri kwa Afrika, ni kweli ameshndwa kuzuia rushwa ndan ya fifa. Bado waafrika watamchagua coz analinda maslah yao na anawadhibit members jeur kama uefa.

Kauli ya Malinz ni kuwa, pamoja na kwamba maofisa wa juu wa FIFA wamekamatwa kwa rushwa, lakin ilikuwa rushwa 'nzuri' maana imepeleka kombe la dunia south afrika, russia na qatar. Ndo maana amemchagua mwenye rushwa nzuri(blatter), kitu ambacho hakingewezekana kama tungekuwa tunachagua kiongoz wa dini.
 
Nafasi nzuri ya kumuondoa Blatter ilikuwa 202 aliposimama na Issa Hayatou wa CAF. Ulaya na mabara mengne hawakutaka kumuamin 'nyani' awaongoze, wakampiga chini, akaishia kupata kura 56 zote bila shaka za waafrika wenzake.

UEFA wamegundua Blatter anapenda madaraka na akiamua asitoke madarakan, hatatoka maana analindwa na kura za afrika na asia. Pia UEFA hawampend Blatter sababu ya sera za 'ujamaa'-mfano sera ya kuipa kila bara nafasi ya kuandaa Worldcup. Kwenye Worldcup kuna mabilion yanatengeneza na ajira za kutosha. Wanapenda sera ya mwenye nguvu ndo ashinde. Pia hawampend kwa kupeleka hela 'zao' Afrika.

UEFA kwasasa hawana namna ya kumuondoa Blatter, labda wagomee kombe la dunia 2018 kama England ilivyotishia. UEFA ikigomea worldcup wataharibu image ya FIFA na kuifilisi kimapato. Lakin ukifikiria ukuaji wa uchumi wa china, hata ulaya wakiremba, makampun ya china yataibeba fifa kwa matangazo. So UEFA watasubir sana.
 
Ktk huu utawala wa JK, moja ya matunda yake ni hii hali ya kuongezeka kwa hisia za kidin. Leo huwez tena ukapiga soga na kutania au kutongoza bila 'kumkwaza' mtu na dini yake. Kwa mujibu wa muktadha wa FIFA, Tweet ya Malinz co ya kidini, ni lugha ya picha. Tumhukumu Malinzi kwa mengine, co hili.
 
Kile cha 2 sided score board ni km €450 tu, kile cha 1 side ni km 370 €

Ndio hapo ujue Jamal Malinzi hafai hata kuongoza kibisa, achana na football association ya taifa. Ye aendelee kulinda maslahi yake tu, sisi na huu uzao wetu tutakufa bila kuona timu yetu ya taifa ikifanya vizuri kwenye mashinda yoyote, acheni watu tuhamie kwenye soka la Ulaya.
 
Hii kauli haikufaa kutolewa na mtu kama yeye.

Inamaana yule jamaa wa Jordan anafaa huko kwenye dini sio mpira?

Hamna Malinzi kaongea ukweli mtupu, wabongo mnapenda kudanganyana na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa, hapo ametoa makavu live kua yuko kule Zurich kwa maslahi ya taifa tu , hayuko kidini kuchagua imam au baba paroko.. mlitaka aume ume eti tu kwa vile ni rais wa TFF..
 
Daah mngekuwa wanafunzi mngechezea stick vibaya. Hiyo ni lugha Ya picha alotumia Jamal Malinzi akimaanisha since hawaendi kuchagua viongozi wa dini! Maadili sio muhimu ndo maana akamchagua mla rushwa Joseph Blatter

umenena vema mkuu
 
Last edited by a moderator:
Vichwa vya watanzania vimejaa udini. Na huo udini umepotosha fikra na ufahamu wa wengi. Hapo Malinzi amempasha mdini aliyejaribu kumshawishi apige kura kwa misingi hiyo.

Maslahi ya nchi kwanza ndio hoja kuu ya rais Malinzi. Sasa udini wake uko wapi?
 
Hakuna shida hapo tungejua alikuwa anajibu nani na juu ya topic gani ndo tungehukumu. Mleta mada angekuja na thread nzima juu ya hili basi tungekuwa ktk wakati mzuri wa kuamua aliimanisha nini kusema hivyo.
 
Daah mngekuwa wanafunzi mngechezea stick vibaya. Hiyo ni lugha Ya picha alotumia Jamal Malinzi akimaanisha since hawaendi kuchagua viongozi wa dini! Maadili sio muhimu ndo maana akamchagua mla rushwa Joseph Blatter

naye kala rushwa...........
 
Vichwa vya watanzania vimejaa udini. Na huo udini umepotosha fikra na ufahamu wa wengi. Hapo Malinzi amempasha mdini aliyejaribu kumshawishi apige kura kwa misingi hiyo.

Maslahi ya nchi kwanza ndio hoja kuu ya rais Malinzi. Sasa udini wake uko wapi?

Mla rushwa tuu ! ...mkabila huyoo ! Nyenyere
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom