Jamal Malinzi ni jipu na anastahili kutumbuliwa kwa maslahi ya taifa

Jamal Malinzi ni jipu na anastahili kutumbuliwa kwa maslahi ya taifa

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,351
Reaction score
2,061
Ndugu,
Kama utakuwa mfuatiliaji wa mpira wa miguu nchini basi si ajabu kwamba katika kichwa chako utakuwa unamkumbuka vema ombwe la uongozi lililofinyanga utendaji wa shirikisho la soka nchini (TFF) tangu Jamal Malinzi madarakani.
Pamoja na mambo mengine, juzi juzi kulikuwa na kashfa ya upangwaji matokeo kwa ligi kuu daraja la kwanza ambapo baadhi ya timu ikiwemo Geita Gold Sports Club kupokonywa ushindi na kushushwa daraja licha ya ushahidi kutokuwa yakinifu ambapo haingii akilini kumfungia mchezaji na kocha msaidizi kwa kudai wamehusika kupanga matokeo pasi na uongozi mzima kuwajibishwa.
Kifupi, utagundua maamuzi ya TFF yalifanyika kwa mhemko uliochagizwa sana na baadhi ya watangazaji wa Cloudz lakini hakuna uchunguzi wa kina uliofanyika.
Pamoja na hayo, ulitolewa muda wa timu zilizoadhibiwa kukata rufaa lakini kabla ya hearing ya rufani, TFF ya Jamal Malinzi imepanga timu kibonde ya Mbao FC ambayo hata kuwasafirisha wachezaji 15 kutoka Mwanza kwenda Geita ilikuwa inapata tabu.
Swali; Rufani Zimepuuzwa?
 
Wanakurupuka tu ndomana kila siku hatupigi hatua tunacheza hapohapo na kurudi nyuma
 
Najiulizaga, wale waliokua wakitokwa povu wakati wa kuelekea uchaguzi kwamba Malinzi ndie anafaa na mazengwe yaliyotokea by then wapo wapi sasa?

The guy clearly has no vision, and I saw it long time ago, ila kwa kelele zile nikarudi nyuma na kutafakari kwamba pengine mimi ndie simfahamu Malinzi na TFF!

Few years down the road, and I am right!
 
alipopanga safu yake tu nikajua amekiwsha
 
Back
Top Bottom