Jamal Malinzi utamaliza vibaya

Majaribu2013

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
952
Reaction score
1,049
Jamal Malinzi,

Kuna kitu kidogo sana ambacho uspokiangalia kwenye uongozi wako utamaliza vibaya na kufuta kabisa kistoria yako ya yale ambayo angalau umeyafanya yanayoonekana ni mazuri.

Mpira wa Tanzania unageuka kuwa vita, chuki, uhasama na fujo kwa UZEMBE wako.
Tangu ligi kuu irejee tena baada ya mapumziko na kombe la mapinduzi nimejifunza kwamba, kuanzia daraja la kwanza na ligi kuu sasa mpira umekuwa wa fujo.

Sasa ni jambo la kawaida kwa wachezaji kupigana viweko uwanjani, kukabana na kutukanana na kibaya zaidi hali inazidi kuwa mbaya lakini hakuna hatua yoyote mnayochukua.

Anzia mechi za daraja la kwanza, njoo kwa Tambwe, njoo kwa Okwi, na hata mechi ya leo ya Mbeya City na Simba Azam TV wameonyesha vizuri ile pepsi aliyopigwa mshambuliaji wa Mbeya city.

Mambo haya yanajenga chuki sana kati ya wachezaji na yasipozibitiwa nakuhakikishia itafikia hatua ya kupigana bastola mitaani maana wataogopa kugombana uwanjani.

Pia maamuzi MABOVU ya marefarii yameshamiri kabisa. Hakuna kitu kibaya na cha kuudhi kama msimamizi (Rais) kuyaona makosa waziwazi na kubaki bubu. Mfano wawazi tu penalt tuliyopewa Simba leo haikuwa penalt hata chembe, mwamuzi aliamua kulipa fadhira ni aibu sana kwa ustawi wa soka letu.


Jifunze haya

1. Angalia chama cha mpira cha Uingereza likitokea tatizo lolote la kutatanisha ni ndani ya masaa 48 jibu litakuwa limetoka kama ni adhabu au onyo. Lakini nyinyi hata mwezi utaisha tu ni aibu sana mdogo wangu.

2. AZAM TV, nadhani moja ya faida za kuonyesha mpira live ni kuweza pia kusaidia utatuzi wa changamoto zinazopatikana. sijui huwa hauangalii hii TV au unaziba macho? Maana hii ndiyo ingewasaidia zaidi kuyaona haya makosa kwa undani kwa kuangalia tukio kwa marudio mengi zaidi.

Naamini mtu ukiwa kiongozi wa jamii yako, ukiona jambo lolote baya moyo wako utashutuka na kulishughulikia haraka haraka. Sasa sijui huwa hauoni au sijui nini?

Kile kitambaa cha Fair Play sikioni siku hizi mara nyingi waliokiwekaga si wajinga kuna kitu huwa kinaingia kwenye mind za wachezaji, tuacheni mazoea.

Ukiyaangalia haya mambo yatakuja kuharibu kabisa historia yako.

Note: Sihitaji utetezi wako ambao kila post huwa haukosi lakini utendaji bado ni wa chini mno, mna ubingwa wa kujibu kwenye media lakini utekelezaji ni sifuri bado. Ukiona kuna cha maana chukua kafanyia kazi.

Ashakumu si matusi.
 
lkn kuhusu malinzi yule bwana hakuna kitu anachojua katika soka nadhani atakaa awamu moja tu na pengine anaweza asiimalize
 
Aibu kila kona kila tulie mtegemea kawa sio na wote ni marais bure kabisa watakuja kuuwana uwanjan maana sio mpira ni vita
 
Hakuna jipya analolifanya amekomaa na frame za maduka wakati soka lenyewe bado liko chini hadi tumekuwa Mashabiki wa Mkopo wa nchi nyingine. #Afcon2015
Discipline hakuna katika soka zima tumeshuhudia hadi wadogo zao katika Madaraka ya chini refa akikimbizwa kama mwizi
 
Naamini katika uchaguzi wowote kila mtu anakuwa na upande. Lakini kwa tuliokuwa upande wa Jamal Malinzi ni kama tunaona AIBU, yaani jamaa ni BOMU kabisa hakuna kitu. Hivi hadi sasa huyu jamaa atajivunia nini kwa muda alioutumia madarakani? Jamal Malinzi hivi kweli wewe ni MTUPU hivi?
 
Jamal Malinzi umeona Diego Costa kafanya kosa juzi tu kwenye mechi ya Liverpool leo kapewa na adhabu. aibu sana kwako.
 
Last edited by a moderator:
Azam tv nao waache unazi siku ya mechi ya simba na azam walikuwa wanakwepa kuonyesha replay ya fauluo aliyofanyiwa okwi llakini ya jana wamerudia mara kadhaa
 
Malinzi alishashindwa kabla hajaanza...na tulionywa kuwa malinzi hana lolote tukawa wabishi..Kutwa yuko twitter na kupanda panda lift za pale PPF towers kuangalia angalia mabebez...soka la TZ linakufa kwa sababu ya Malinzi

Yaani sijui huwa wanatafuta nini? anapigana wee anaahidi mambo mengi mwisho wa siku akifika sifuri kabisa.
 
Nilianza kuudharau uongoz wa Jamal Malinzi pale tff tangu ile siku wanamuidhinisha Emanuel Okwi kuwa mchezaji halali wa simba kutoka yanga. Inaniuma sana kumuona kijana mwenzetu anafanya mambo hovyo namna hii. Leo watz tupo busy kuangalia congo brazaville wakitesa afcon, cape verde hawa hawa ambao walikuwa hawachomoki kwa watz leo hii wenzetu wametuacha mbali kabisa, JAMAL MALINZI ana mipango lukuki kwenye makaratasi lakin utekelezaji 'F'.
 
Nimegundua kwanini Leodga Tenga alimkataa sana Malinzi...ni mtu asiyejua lolote kuhusu soka..
1-Kusitisha makataba ghafla kwa kocha wa timu ya taifa....(chuki na uongozi uliopita)
2.Kusaka vipaji kwa njia bonanza.(kukosa ubunifu)
3.Timu ya taifa(maboresho)kuundwa na wachezaji wasio na vilabu..(kukosa mipango ya mda mrefu)
4.Kuhamisha ofisi za TFF hadi PPF(siyo mchumi...na kutia hasara chama)
 
Tuache personification, TFF ni chombo cha Watz na sio cha JM, yeye amechukua dhamana kwa niaba yetu, hii mada imetoka kaa laanio, tuendelee kumshauri na kumtia nguvu JM, ameunda vyombo mbalimbali vya kumsaidia navyo pia vishauriwe kwa namna ya pekee, mfumo wa EPM ni tofauti kdg na kwetu huku, waamuzi wanachezesha kwa kutumia macho makavu na si sayansi ya kiwango cha lami kama EPM etc...anyway hoja yangu ibaki kwamba tumshauri Rais na ameanzisha uzi wa kumshauri na tukosoe bila kunyoosheana vidole ..........silent is gold while speech is silver
 
vipi Yanga alipoidhinishwa kuchezea Yanga, umbumbu wa viongozi wako usiwe ni scape goat
 
lkn kuhusu malinzi yule bwana hakuna kitu anachojua katika soka nadhani atakaa awamu moja tu na pengine anaweza asiimalize

anajitengenezea mazingira ya kuingia siasa.
 
vipi Yanga alipoidhinishwa kuchezea Yanga, umbumbu wa viongozi wako usiwe ni scape goat

Ndo matatizo yenyewe hayo na mengine ndugu, usilete hoja za kishabiki wewe!!! Kumbe hata na wewe bure tu?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…