Majaribu2013
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 952
- 1,049
Jamal Malinzi,
Kuna kitu kidogo sana ambacho uspokiangalia kwenye uongozi wako utamaliza vibaya na kufuta kabisa kistoria yako ya yale ambayo angalau umeyafanya yanayoonekana ni mazuri.
Mpira wa Tanzania unageuka kuwa vita, chuki, uhasama na fujo kwa UZEMBE wako.
Tangu ligi kuu irejee tena baada ya mapumziko na kombe la mapinduzi nimejifunza kwamba, kuanzia daraja la kwanza na ligi kuu sasa mpira umekuwa wa fujo.
Sasa ni jambo la kawaida kwa wachezaji kupigana viweko uwanjani, kukabana na kutukanana na kibaya zaidi hali inazidi kuwa mbaya lakini hakuna hatua yoyote mnayochukua.
Anzia mechi za daraja la kwanza, njoo kwa Tambwe, njoo kwa Okwi, na hata mechi ya leo ya Mbeya City na Simba Azam TV wameonyesha vizuri ile pepsi aliyopigwa mshambuliaji wa Mbeya city.
Mambo haya yanajenga chuki sana kati ya wachezaji na yasipozibitiwa nakuhakikishia itafikia hatua ya kupigana bastola mitaani maana wataogopa kugombana uwanjani.
Pia maamuzi MABOVU ya marefarii yameshamiri kabisa. Hakuna kitu kibaya na cha kuudhi kama msimamizi (Rais) kuyaona makosa waziwazi na kubaki bubu. Mfano wawazi tu penalt tuliyopewa Simba leo haikuwa penalt hata chembe, mwamuzi aliamua kulipa fadhira ni aibu sana kwa ustawi wa soka letu.
Jifunze haya
1. Angalia chama cha mpira cha Uingereza likitokea tatizo lolote la kutatanisha ni ndani ya masaa 48 jibu litakuwa limetoka kama ni adhabu au onyo. Lakini nyinyi hata mwezi utaisha tu ni aibu sana mdogo wangu.
2. AZAM TV, nadhani moja ya faida za kuonyesha mpira live ni kuweza pia kusaidia utatuzi wa changamoto zinazopatikana. sijui huwa hauangalii hii TV au unaziba macho? Maana hii ndiyo ingewasaidia zaidi kuyaona haya makosa kwa undani kwa kuangalia tukio kwa marudio mengi zaidi.
Naamini mtu ukiwa kiongozi wa jamii yako, ukiona jambo lolote baya moyo wako utashutuka na kulishughulikia haraka haraka. Sasa sijui huwa hauoni au sijui nini?
Kile kitambaa cha Fair Play sikioni siku hizi mara nyingi waliokiwekaga si wajinga kuna kitu huwa kinaingia kwenye mind za wachezaji, tuacheni mazoea.
Ukiyaangalia haya mambo yatakuja kuharibu kabisa historia yako.
Note: Sihitaji utetezi wako ambao kila post huwa haukosi lakini utendaji bado ni wa chini mno, mna ubingwa wa kujibu kwenye media lakini utekelezaji ni sifuri bado. Ukiona kuna cha maana chukua kafanyia kazi.
Ashakumu si matusi.