Jamal Musiala mchezaji mwenye kipaji sana

FK21

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2019
Posts
8,600
Reaction score
10,760
Wakuu habari za mda huu.
Ni ukweli usiopingika kuwa vipaji katika mpira huja na kupotea. Lakini kinachosikitisha ni watu wa zamani kupendelea ukale wao na kuamini kila aliecheza zamani alikuwa anajua mpira.

Hilo apo juu ni povu langu muache kukumbati ukale. Hivi kuna mtu amejaribu kumfuatilia kwa ukaribu uyu (Muislam Mjerumani) anaekipiga katika club ya Bayern Munich, kijana Jamal Musiala?

Kama hujawahi kumfuatilia, jaribu kumfuatilia. Kijana anajua sana mpira, ukifuatilia hakika utaamini kuwa OUR FOOTBALL IS IN SAFE HANDS.
 
Watu wa zamani wanazungumziwa sababu walifanya makubwa waliweza kudumu kwa kiwango chao kwa muda mrefu, sasa unataka jamal musiala azungumziwe sawa na gaucho, ama kina maradona? Yeye afanye yake atazungumziwa akifeli hakuna mtu atamzungumzia, hata hao wa zamani kuna ambao hawazungumziwi.
 
Imani yangu inaniambia wachezaji wa Sasa ni Bora kuliko wa zamani
 
Yah Yuko vizuri sana

Pia ukipata mda mfwatilie jamaa mmoja anaitwa Sheraldo Becker yupo Union Berlin ni hatari sana.
 
Kulikuwa Kuna haja Gani YA kuandika Dini yake? Mbona mna inferiority complex nyie watu?
 
Waingereza wanajuta kumuachia huyu dogo kua mjerumani. Maana hadi kufikia mwaka 2020 alkua anachezea uingereza U21..sasa ivi ndo anakiwasha balaa.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Umeeleweka sheik
 
Yah Yuko vizuri sana

Pia ukipata mda mfwatilie jamaa mmoja anaitwa Sheraldo Becker yupo Union Berlin ni hatari sana.
Navyokuheshi nitamfuatilia
 
Imani yangu inaniambia wachezaji wa Sasa ni Bora kuliko wa zamani
Zamani kulikuwa na wabovu na wazuri, hata sasa kuna wazuri na vimeo.

Ukisema wachezaji wa sasa umeanzia wa mwaka gani, Ronaldo de lima wa sasa ama zamani, gaucho je.. Kina baggio? Zidane.. Nifahamishe hapo.
 
Chelsea alumni huyu! Walimuuza kwa bei mbuzi! Leo anafanya mambo makubwa na Bayern Munich! Huku wenyewe ikiendelea kuokoteza wazee kama Aubemyang.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…