bornagain
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,383
- 1,357
Mimi nadhani KIZUGUTO ni mtu sahihi pale TFF tatizo mnadhani kitengo cha habari cha TFF kinahitaji mtu mwenye uwezo pekee wa kuandika habari au kuwa mtangazaji mnasahau kuwa TFF ina website na mtu wa habari ukipata ambaye pia ni mtaalamu kwenye tekinohama unakuwa umepiga ndege wawili kwa jiwe moja, huyu Kizuguto kafanya vizuri sana pale Yanga hasa kwenye ishu ya WEBSITE maana website yao ilikuwa updated kuliko website ya Club yoyote Tanzania na ukitaka kuamini hilo ingia website ya Yanga leo update ya mwisho ni siku chache kabra ya kizuguto hajaondoka Yanga huyo aliyeingia sasa hivi (Jerry Muro) kutwa kuongea kwenye press conference website zero, hivyo nadhani TFF wameliona hili ukizingatia na wao Website yao ipo hoi bin taabani lakini ukiacha hilo huyu kizuguto nimekuwa nikimsikiliza amejipambanua kama msemaji anayeongea kwa weledi si kuropoka kama wasemaje wengine.
Kwa hiyo wamemuajiri kwa ajili ya website, mimi najua website ni ya watu wa IT sasa kama yeye anafanya vyote ina maana TFF hawana IT