Jaman ..hivi ni kweli

Jaman ..hivi ni kweli

Andrew Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
330
Reaction score
117
Kuna mambo ambayo mpaka sasa nashindwa kujua nfanyeje...jaman mliooa au mnaolijua hili nambieni, kuna umuhimu wa kuoa mke uliyemzidi umri?
 
Kama una akili ya kiume ni sawa, kama ni baby boy usijaribu.

Afu mnapishana miaka mingapi?
Mambo ya watu kuwa wanadhani mie mama ako sitaki lol
 
Kuna mambo ambayo mpaka sasa nashindwa kujua nfanyeje...jaman mliooa au mnaolijua hili nambieni, kuna umuhimu wa kuoa mke uliyemzidi umri?

Cha muhimu ni kuoa mke anaekupenda kwa dhati, umri hauna nafasi kwenye mapenzi
 
Ni muhimu sana tena sana, kuoa mke ambaye umemzidi walau 3 or more years. Ukipata ambaye unamzidi 5-10 yrs ni bora zaidi.

Kama unahitaji maelezo zaidi tutafutane,

Babu DC!!
 
Ni muhimu sana tena sana, kuoa mke ambaye umemzidi walau 3 or more years. Ukipata ambaye unamzidi 5-10 yrs ni bora zaidi.

Kama unahitaji maelezo zaidi tutafutane,

Babu DC!!

hyo ilikuwa zamani bana babu DC, kinachotakiwa ni upendo na heshima tu
 
Kuna mambo ambayo mpaka sasa nashindwa kujua nfanyeje...jaman mliooa au mnaolijua hili nambieni, kuna umuhimu wa kuoa mke uliyemzidi umri?

Tangu tunakua, tumejikuta Waafrika wengi tuko kwenye tamaduni ya aina hiyo. Nilikuwa nasoma vitabu vingi vya zamani, vilikuwa vikisimulia kuwa ilikuwa inafikia level ya mtoto wa kike anapozaliwa hapo hapo anakuwa "booked" kuja kuolewa na kijana au mzee fulani!

Lakini ki ukweli, huu ni kama utamaduni tu wa zamani ambao kimsingi huufanyi kazi kwa nguvu ile ile kwa vijana wa kizazi cha sasa. Ki ushauri, niungane na huyo mchangiaji hapo juu kuwa suala muhimu ni kupendana kwa dhati. Suala la umri lisiwe kikwazo sana ingawa pia unatakiwa kuwa na mipaka ya huo utofauti wa umri.

Si busara we kijana kuoa/kuolewa na kibabu/kibibi. Kwa mtazamo wangu naona tabia, interest na hulka zinaweza kupishana na hivyo kuleta migogoro isiyo ya lazima.

Thanks,

HP
 
Cha muhimu ni kuoa mke anaekupenda kwa dhati, umri hauna nafasi kwenye mapenzi

hyo ilikuwa zamani bana babu DC, kinachotakiwa ni upendo na heshima tu

Kwa heshima yote inayokustahili bigi braza,
Its undeniable fact kwamba Love is the foundation...Ila kubadilika kwa nyakati bado hakuondoi changamoto za kisaikolijia zinazosababishwa na kutofautiana sana kwa umri kati ya wanandoa..
So, You also think its a mere coincidence that marriages of these times are not stable in comparison to those before these times?
 
Kwa hyo glory ndo amekuzid umri sio?
 
Back
Top Bottom