Mkuu heshima japo umekuwa specific kwa chuo kimoja ila unatakiwa kutazama mfumo mzima Tanzania. Suala la rushwa ya ngono ni kweli ipo na imejaa tele kwenye taasisi za elimu ya juu. Lakini si kwenye taaisis hizo tu hata serikalini watu siku hizi wanapeana vyeo kama malipo ya ngono.
Tukirudi katika taasisi za elimu ya juu. Ni dhahiri kabisa kuwa wanaosoma huko ni watu wazima wenye kujua wajibu wao na kujitambua katika jamii. Sasa mtu mzima anapolalamika kuwa amelazimishwa ngono kwa kutishwa basi huo tunauita ni ubakaji, na anastahili kumfikisha mtuhumiwa kwenye vyombo vya dola, ila kama atabakia kimya basi ni dhahiri ameridhia kitendo hicho. Ninachokiona katika post yako hii ambayo inakosa connection to the point on whether the weak management is the source of the practice or lack of ethics among academicians as well as students but no clear explanations from your post.
Mimi nimepitia pale UDSM miaka ile ya Mmari, tatizo hili lilikuwepo na ninakumbuka kuwa ilifikia hatua baadhi ya wanafunzi wenzetu wa kiume walikuwa wakigombana na baadhi ya wahadhiri kwa kuwa wapenzi wao wa kike walikuwa wakichukuliwa na wahadhiri hao. Nina hakika kabisa kuwa ingekuwa enzi hizi za utandawazi basi tungeshuhudia posts kama hizi kutoka kwa wanafunzi waliojikuta wanachangia wenza na walimu kwa kuwaanika hadharani as part of the fracas.
Tatizo la ngono kwenye mjumuiko wa watu wazima halikwepeki, nenda bungeni, nenda serikalini na maofisini, nenda shule za sekondari, nenda vyuoni. Kinachotakiwa hapa ni kuwa na miiko na kufuatiliwa ili anayeivunja apate adhabu stahili. Kama wachangiaji walivyosema njia pekee ya kuwa salama ni kufuata kilichokupeleka chuoni, yaani soma kwa bidii na fuata maelekezo mwisho wa siku utafaulu mtihani wako bila msaada wa rafiki, boyfriend, au lecturer. Ukifuata mob saikoloji ujue kuwa mitihani itafika ukiwa huna kitu kichwani ni hapo utakapojikuta unakuwa mtumwa wa ngono ili upitsihwe. Kama umeingia darasani na kujifunza mbili mara mbili ni nne, ni dhahiri ikija kwenye mtihani utajaza nne na hakuwa wa kukukosesha eti kwa kuwa umemnyima ngono.