Jamani anataka kufia bungeni huyu tumwokoaje??

Wana saikolojia wansema sisi wote kama binadamu tuna kichaa. Kila mtu ana kichaa chake fulani tangu anakua mtu mpaka unakufa. Mrema ana ukichaa wa kupenda madaraka. Ndio kichaa chake!

Mkuu motive ya mwanasiasa yeyote ni madaraka. Zaidi ya hapo huyo sio mwanasiasa ila anaganga njaa kama walivyo baadhi ya viongozi wa tz.
 
mwacheni agombee, kwani mmeona aliyezeeka ni mrema peke yake humo bungeni? mbona kuna vijana wanakaa tu wanapiga miayo hawachangii chochote na hamsemi? yaani mnamuona huyu huyu tu? kwanza wapiga kura wake ndo wamemuita agombee so? bora uwe na mzee mrema bungeni kuliko kuwa na wabunge vijana wavivu hata kuchangia mswaada hawawezi, hata mkiwafundisha wakifika kule washasahau kila kitu, wanasuri posho na jioni kwenda maili mbili ya chako ni chako pale kula maini ya mbuzi.

mrema bravo brother, tunataka changamoto mpya tumechoka na bunge hata kusikiliza halina msisimko. mi nakufagilia mzee wa kilalacha - big up mbele kwa mbele.

Nakuja huko kukupigia kura - ila sijajua jimbo letu wanamleta nani kuja kukumaliza maana moshi mjini limepata mtu tayari - tutamsubiri kwa hamu
 
Hivi wana JF siyo kwamba ni haki ya mtu yoyote kuamua kugombea ubunge as long as chama chake kimemruhusu kuingia kwenye ungombea huo wa ubunge?
 
Mvina
Mrema wala hahitaji kuboresha maisha yake kwani anafahamu kwamba ana muda mfupi sana wa kuishi hapa duniani.Anataka kuwa Mbunge ili azikwe vizuri na si vinginevyo.

Kauli yako inanipa utata kidogo. Umetumia formula gani kujua kwamba anamuda mfupi wa kuishi? au maisha yake yako mikononi mwako? Je wewe ndiye mungu wake aliyempa uhai?
Kuwa mzee si sababu ya kufa mapema. Yawezekana wakafa vijana na watoto wengi wakamwacha mrema bado yungali hai.
Mtu kuzikwa vizuri akutegemeani na ubunge bali inategemeana na yeye aliishi vip na watu na alitoa mchango gani kwa watu hao.
 

That actually a really good answer to so many of these people here. Watu hapa wanaongea sana pumba, na ndio maana mi nasemaga Watanzania wakati mwingine ni kama mbumbumbu wa hela na heshima za kijinga... Tunajudge watu kama sisi ndio Mungu na tunajua lini na wapi mtu anakufa.. Hivi kwa stahili hii tutaendelea Tanzania? Watu wanasema kwamba mrema amechacha kuna mtu yoyote amewahi kuiona bank statement yake, au wana any kind of evidence kuwa hawezi kula au kulisha familia yake? Tatizo kubwa mimi nilionalo hapa ni kwamba watanzania tumezoea kuona matajiri na Political leader wako kwenye Vx na tunaamini kwamba wanahela au wanamaisha manzuri. Mtu akiwa wa kawaida kama afanyavyo mrema wanaoana amechacha. Kwa hizi fikra zetu sijui kama economy yetu inaendelea kabisa!!!
 
kumbuka umri na afya yake na ujue hata kingunge kuna wakati alikuwa na busara kabla hajapa ugonjwa wa uzee

ndugu wewe ni medical doctor? Una any evidence kwamba afya yake itamtatiza kutenda kazi yake? Mbona JK ameanguka mara kadhaa na anatenda kazi zake za kuzurura?Mimi binafsi naamini kwamba kama watanzania tunataka ufisadi ufichuliwe bungeni tunaitaji watu watakao simama bila kumuogopa mtu na kutoa point that include mrema. Wabunge tulionao sasa ni wanaenda kufanya utalii tungeni..
 
- Mrema atachangamsha mawaziri wa CCM, maana hana uoga muacheni agombee anaonekana bado ana some gass kwenye tank!

Respect.


FMEs!
 
Bwana weh, haamini hivyo... anajua watu wanampenda na watamchagua hata kuwa rais akitaka!!

Hivi chama chake kina hali gani kwa sasa?


chama chake kina hali nzuri, inategemea unaangalia from which perspective. . .
 
Hawezi kuungana na wapinzani wenziwe katika kuibana serikali kuhusu ufisadi.

Nyie mtamuona tu mzee huyu.

Mkuu tutamuona wapi? Mbona imesheleweka harudi mjengoni, kwa hiyo hakuna sehemu ya kumuona.
 

Habari zisizo rasmi zinasema huyu mzee ni pandikizi la CCM kwenye upinzani ili kuuvuruga. Na kweli ukiangalia waweza kuamini kwani mzee huyu aliivuruga NCCR iliyokuwa tishio enzi zile kabla hajahamia TLP. Pia mara zote mzee amekuwa hakubali kuungana wapinzani kuwa na mgombea mmoja vinginevyo kwa sharti ya kwamba yeye ndo awe mgombea. Huenda hii ya sasa ikawa ni njia mojawapo ya kuwanyamazisha hao wapiganaji dhidi ya ufisadi akiwemo Kimaro. Kingine ni kuwa mzee huyu ni usalama wa taifa na kama wewe ni usalama wa taifa na ukaonekana unakwenda kinyume na taratibu zao wanaweza kuku-Kolimba.
 
sio kwamba nasema kuwa Mrema ni bora lakini mi nasupport sana viongozi wengi wa vyama vya upinzani warudi majimboni kugombea ubunge kwani wakiwa bungeni basi labda kuna kitu kitafanyika.we fikiria tungekuwa na kina Kabwe kama kumi hivi ambao wako bungeni mambo yangekuwaje.mi nadhani akirudi bungeni anakuwa na faida zaidi kuliko kukaa kama alivyo sasa hatusikii akifanya chochotye,kwani utaniambia na hao walio na afya zao wamefanya nini bungeni?
 
Watanzania hapa ndipo mimi ninafika mahali ninashangaa maono yaliyo ndani yetu. Hivi tangu miaka 20 ya awali ya Mrema + Hii ya Kimaro ambay inadaiwa hajafanya jambo lolote la maana; HAKUNA WATANZANIA WENYE MWAMKO MPYA AMBAO WANAWEZA KUNG'OA HAWA WABABAISHAJI WA KISIASA?. Tuamke sasa, tunahitaji sura mpya, zenye mwamko. Sura nyingi ninazoziona JF zikitoa michango yao ya mawazo; inadhihirisha vipawa vizuri ambavyo vinaweza kuleta mabadiliko ktk jamii yetu. Si wakati wa kuendelea kusubiri watu waliocheza mpira miaka ile ya akina Masatu. waje wacheze ktk taifa stars (The Blues of Afrika) ya akina Tegete!!. Tutaendelea kufilisika!!.

Tuinuke sasa, tufunge buti!


Si vyema kuona udhaifu wa mtu kiafya alionao sasa hivi ukadhani atakufa leo au kesho!. Wakati fulani hatunabudi tupities katika udhaifu fulani na pindi tunapoinuliwa na Mungu, hutengeneza historia.

Kama hakuna wa Tanzania wengine kule Vunjo, walioamka, mwacheni mrema akagombee Ubunge, wala msimtolee maneno ya kejeri wala matusi wala macho mekundu!. Ni haki yake kama raia. Nani kaiona kesho? Tunatembea hali kesho yetu imefunikwa na pazia, hatuwezi kuiona! tusishutumiane kwa sababu leo afya zetu zinateteleka! Kesho yaweza kuimarika na tukafanya mambo makubwa yasiyokuwa ya kawaida! Nani alijua F Castro atakuwa hai mpaka leo au yule ndg aliye achiliwa huru wale wa western wakidhani hatamaliza hata wiki 2!!

Kimaro kama amefanya kazi inayoonekana asiogope!
 
Mrema ni mtu muhimu sana, bado tunahitaji mchango wake bungeni, hajaanza kupoteza kumbukumbu kama wazee wengine pale mjengoni hasa yule anayeipenda na kuisifia ilani wa wakatoriki...ha ha ha

Vunjo bwana tumemwita rasmi aje kumalizia kazi na atuage rasmi, kwetu vunjo mrema ndo kamanda wetu, hata aje ki vipi ila kura analamba zootee, - na wale wenzetu wakija na kofia na furana na bakshishi zao tunalamba na siku ya uchaguzi tunatoa majibu.

nani asoujua mchango wa mzee wa kiraracha? kumbuka enzi za sungusungu chief, kumbuka zile siku saba saba, mawaziri na watendaji serikarini wengine waliamua kuacha kazi mchezo, kwangu mimi naona bado anahitajika in next 10 years.

Kuna jamaa hapa atasema "hatuishi kwa kukumbuka za mambo ya zamani" ha ha ha, ila namkumbusha mbona akiomba kazi anatoa CV, sasa CV ni nini?


Mrema jiandae nasikia wanamleta mtu kuja kukumaliza vunjo - tayari pale Moshi mjini washatuma kamanda wao kummaliza ndesa mshiko na ameshaweka kambi pale hadi 2010 siku ya uchaguzi - jiandae

Mwisho wanaokufuatafuata hao ni si si emu, hawataki uendelee, wamesahau ulivyowagaragaza pale temeke ha ha ha

nipo nyuma yako kamanda - HADI KITAKAPOELEWEKA.... ila nakuchauri uje chadema ili tuunganishe nguvu unaonaje?

porojo tu mjombaa, simaanishi ivyo....
 
Huyu ni Ze Komedi, nafikiri anachekesha wenye mapendo. Huyu atamuwakilisha nani sasa? nafikiri mmuelewe kwamba anachangamsha jukwaa la wanasiasa.
 
Wakuu nlikua Vunjo hukpo week end hii. Nimefanya mahojiano na baadhi ya wanazi wa siasa za pale na nimetembelea maeneo mbalimbali ya jimbo hili Eg, Marangu, Mwika,Himo, Kirua vunjo na Uchira. wakuu Mbabu bado ananguvu na haitashangaza akikamata.

Just tuchukue takwimu za serikali za mitaa, TLP wameibuka kidedea off all upinzani huku na wameongeza viti lukuki. Juzi Kimaro kazomewa himo kama mtoto, katukanwa kapawa mbayaaa. wazee hawataki muona.

Kwakweli upinzani ikitaka jimbo hili lirejee wampe nguvu mzee huyu maana anakubalika naimani kuliko mpinzani yeyote kule. Ni msema hovyo, mropokaji ndio, lakini tunawahitaji sana waropokaji huko bungeni, wanaojiita walipua mabomu. Ili pale Dom pawe pachungu. Bora mare dufu tumuunge huyu mzee mkono arejee kuliko kuendelea kuliach hili jimbo chini ya mikono dhalimu ya CCM.

Yetu macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…