Mrema ni mtu muhimu sana, bado tunahitaji mchango wake bungeni, hajaanza kupoteza kumbukumbu kama wazee wengine pale mjengoni hasa yule anayeipenda na kuisifia ilani wa wakatoriki...ha ha ha
Vunjo bwana tumemwita rasmi aje kumalizia kazi na atuage rasmi, kwetu vunjo mrema ndo kamanda wetu, hata aje ki vipi ila kura analamba zootee, - na wale wenzetu wakija na kofia na furana na bakshishi zao tunalamba na siku ya uchaguzi tunatoa majibu.
nani asoujua mchango wa mzee wa kiraracha? kumbuka enzi za sungusungu chief, kumbuka zile siku saba saba, mawaziri na watendaji serikarini wengine waliamua kuacha kazi mchezo, kwangu mimi naona bado anahitajika in next 10 years.
Kuna jamaa hapa atasema "hatuishi kwa kukumbuka za mambo ya zamani" ha ha ha, ila namkumbusha mbona akiomba kazi anatoa CV, sasa CV ni nini?
Mrema jiandae nasikia wanamleta mtu kuja kukumaliza vunjo - tayari pale Moshi mjini washatuma kamanda wao kummaliza ndesa mshiko na ameshaweka kambi pale hadi 2010 siku ya uchaguzi - jiandae
Mwisho wanaokufuatafuata hao ni si si emu, hawataki uendelee, wamesahau ulivyowagaragaza pale temeke ha ha ha
nipo nyuma yako kamanda - HADI KITAKAPOELEWEKA.... ila nakuchauri uje chadema ili tuunganishe nguvu unaonaje?
porojo tu mjombaa, simaanishi ivyo....