Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Leo asubuhi nimeamka na hamu ya BAGIA ZA IRINGA, hasa za KALENGA!, liliko fuvu la Chifu Mkwawa aliyekuwa kiongozi wa Wahehe aliyepinga ukoloni wa Kijerumani mwishoni mwa karne ya 19 kabla ya kujiua mwaka 1898 ili kuepuka kukamatwa.
Tuachane na ishu za historia maana isije ikawa ni chenga ya maudhi kwa hawa GEN Z, acha niendelee na michapo ya hizi Bagia za Kalenga, vitafunwa vya kitamaduni, vinavyotokana na Kunde, ambapo hutiwa viungo (chumvi n.k), kisha kukaangwa hadi kuwa na rangi ya kahawia na kuwa na ukoko wa nje.
Utake mwenyewe ule bila pilipili au ule na kiungo hicho ili kuongeza ladha.
Kutokana na umaafuru wake Bagia hizi kupikwa Kalenga na kusafirishwa mapema alfajiri Iringa mjini umbali wa km 14.6, na kuwauzia wasafiri mbalimbali kwenye vituo vya mabasi.
Hii ni moja ya biashara kubwa kwa kina Mama, na wamekuwa wakitengeneza kipato kwa ajili ya familia zao.
Soma ==> Historia ya Mkwawa na Uhehe