Biashara hii yahitaji usimamizi mkubwa sana,kwanza kuwa na mkataba na Dereva means pia mwisho wa mwezi atakuwa na mshahara,mwache awe huru mwenyewe kutafuta konda wake ila wewe utadili na yeye tu,nunua vitu vyako kwaajili ya service na chagua siku maalum ya kufanya service,mfano mi hufanya Service jumapili ,hakuna gari yyt kufanya kazi jumapili ni siku ya service na yupo fundi maalum,service ndogo anahusika dereva,service kubwa zinakuhusu tajiri. Dereva kabla ya jumapili atakwambia kesho yake anaservice gani na gani,ataleta hesabu mliyokubaliana kwa siku mi hiyo siku ya service ndo huleta hesabu ya wiki nzima yaani siku 6. Kuwa na mkataba wa kutokuendesha nje ya root na iwapo atafanya hivyo kazi hana na litakalomkuta atawajibika,so means makosa yote ya kizembe ya barabarani sijui traffic kafanyaje anahusika yeye,labda itokee imekamatwa mfano bodi imechakaa,au viti vimeharibika na aliniambia sikutake action hapo nitawajibika mimi. Kuwa na muda maalumu wa kupaki gari,kama kupaki gari ni saa mbili usiku iwe hivyo siku zote labda itokee ana tenda maalum.
Mkataba wa kazi ndo kiongozi wako,itakuongoza wewe,itamuongoza dereva itamfanya kuwa mwaminifu kwa kazi yake na kuipenda na ataipenda gari,kuwa mtu mwenye msimamo na serious haswaa hasa kwenye swala la pesa na uzembe. Lakini pia kuwa friend kwao siku moja moja cheer up with them wanapofanya vizuri mpe bonas hata buku 10 sikiliza matatizo yao,solve them. Utaishi vyema sana yaani mimi nina madereva wengine huu ni mwaka 6 hata sijabadilisha na ninapoongeza gari wao wenyewe wanakuwa wa kwanza kunitafutia faithfully person,hesabu yangu kwa mwezi kama kawaida ile ile expected na Mungu akibarikia uharibifu mkubwa hujatokea kwenye gari basi ni bam bam. Kikubwa magari yanatakiwa uyapende uyafanyie service za ukweli usiwe mbahili utainjoi sana,mambo ya kubadilisha oil ziwe kama ilivyopangwa kwa kilometre zile zile,penda kunotis utofauti wowote unaouona kwenye gari jua umetokea kwasababu gani siyo unaona tatizo unalifumbia macho,na kama dereva yeye aliona anasikia kila siku hakusema atakuwa responsible kwa uzembe huo. Usikate tamaa pambana utatoka ni biashara nzuri hutajuta.