Hapa mtaani kwetu wamekuja jamaa flani si vyema kuwataja jina ila wana Mobile Clinic. Wanasema wana mashine ambayo haihusishi kutoa damu, yani unaweka mgono tu inafanya full body checkup.
Zinaitwa SU machines; watu wanakimbilia hatari, mpaka wanapanga foleni! Hivyo nimeona bora kupata maoni ya wadau manake naona familia yangu pia inataka kushawishika kwenda!