Jamani hapa kuna ukweli au sanaa (utapeli)?

Jamani hapa kuna ukweli au sanaa (utapeli)?

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,164
Reaction score
1,293
Hapa mtaani kwetu wamekuja jamaa flani si vyema kuwataja jina ila wana Mobile Clinic. Wanasema wana mashine ambayo haihusishi kutoa damu, yani unaweka mgono tu inafanya full body checkup.

Zinaitwa SU machines; watu wanakimbilia hatari, mpaka wanapanga foleni! Hivyo nimeona bora kupata maoni ya wadau manake naona familia yangu pia inataka kushawishika kwenda!
 
Step by step

Hamna lolote hapo mkuu, tena siku hizi watu wanaojiita ma dr. Fake ndio wanaozitumia sana kwenye vi hospital vyao, unakishika mkononi kama ki tube fulani hivi kinaunganishwa kweye ki mashine chake kama ki laptop baada ya dk kadhaa eti kina kupa matatizo yaliyomo kwenye mwili wako!!!! Ni vingi sana siku hizi hasa kwa hawa tiba mbadala
 
Last edited by a moderator:
test-your-stupidity.jpg

Hiyo inaendana na hii, hakuna kitu kama hicho.
Ni Tanzania tu unaweza kuta vitu vya namna hiyo
 
basi wazaramo wa watu huku pwani mpaka wanapanga foleni kupata vipimo wanaliwa hela balaa
 
Gharama zao zikoje?

wanasema ni bure ila ukifika wanakusajili kwenye daftari lao unalipa sh elfu tano ndo unaingia kwenye kipimo hapo ndo kwenye kazi

kuna jamaa zangu wawili wamepima baada ya kulipa elf tano wameambiwa wana maradhi mengi sana hivyo mmoja kaambiwa atoe 280,000 na mwingine 250,000 ndo wapatiwe dozi wote wameshindwa. Nafkiri hawa lengo lao ni hizi elfu tano
 
Duniani kote sijaona kipimo kinachoweza kugundua maradhi yote. Madaktari makanjanja hao.
 
Back
Top Bottom