laussane
JF-Expert Member
- Oct 8, 2009
- 255
- 132
- Thread starter
- #41
Duu, wengi mnamlaumu Laussane hakusoma alama za nyakati, mapenzi ni upofu nyie, ohooo!
...Huyo mwanaume ndio wa kulaumiwa kwa undumilakuwili wake. Hana msimamo kabisa huyo Ndugu. Anaoa kwa matakwa yake au ya ndugu zake? wanaume wengine bwana...
Laussane, maisha ndivyo yalivyo. Kuna mengine mpaka yakukute ndipo utaamini sio hadithi za kutungwa...
Ipo mifano mingi watu wa namna hiyo, kuna dada ambaye alikuwa na mchumba'ke ughaibuni ambaye alikuwa anamhudumia kila kitu, kuanzia nyumba, fenicha, mahitaji ya ndani, usafiri na pesa za matumizi, akitaraji siku akirudi atafunga naye ndoa... kumbe Mwanamke huyo kamweka kinyumba njemba mwingine...
By the time jamaa wa ughaibuni anarudi kuja kuoa, anakuta 'mchumba' kwenye hatua za mwisho mwisho kufunga ndoa na njemba, tena wakati huo ana ujauzito mkubwa tu...
Visa hivi vya kudanganyana vingi sana, ...pole kwa yaliyokukuta. La msingi mwambie hakuna ndoa ya siri, kama anataka ndoa awashirikishe wazazi wa pande zote mbili, ili utambulike kisheria na kidini (ikibidi), na huyo mtoto atayezaliwa apate haki zake.
Mbu
Asante sana nimekusoma ushauri wako uko juu vibaya mno, ubarikiwe