mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,682
- 10,801
Juzi juzi nimeenda CRDB bank kuomba mkopo, ile ya wafanyakazi, baada ya kusikia wameshusha interest rate toka sijui ngapi hadi 17 or 18 (sikumbuki vizuri). Nilipofika nikapokelewa vizuri na nikafanyiwa hesabu ya kiasi cha mkopo nachoweza kuchukua (at maximum) kulingana na salary slip yangu. Baada ya kujua kiasi cha mkopo nikataka pia kujua breakdown ya makato ya kila mwezi for 4 years. Hapa ndo nilikata tamaa kabisaaa! manake baada ya kufanya hesabu nikajikuta mwisho wa miaka 4 nitakuwa nimerejesha fedha zao plus nusu ya hizo fedha tena! Sasa nikajiuliza kwanini wanatangaza kuwa interest rate ni 17 sijui 18 whatever wakati uhalisia ni 50 au nearly 50%????
Jamani naombeni uzoefu wenu pengine nimejichanganya mwenyewe! manake nahisi kuishiwa nguvu na hii mikopo, loh!
Jamani naombeni uzoefu wenu pengine nimejichanganya mwenyewe! manake nahisi kuishiwa nguvu na hii mikopo, loh!