Jamani hii ndoto inamaana gani?

Jamani hii ndoto inamaana gani?

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,621
Hapo vipi!

Jana nimeota passport yangu ya kusafiria nimekuta mahali imetupwa na imekanguliwa na wembe maandishi yote kwenye passport kisha ikakatwa kipande.

Nina imani huku kuna watu wana karama ya kufafanua ndoto na kusaidia.

Naombe msaada wa maombi yenu.
 
Umeshafungwa njia zako...

Bwana alisema atakubariki uingiapo na utokapo...
 
Ndoto huwa ni mawazo yanayojirudi kwa kile unachokifikiria.

Wakija watu wa imani hapa, watakutisha. Kwa ushauri wangu, leo kula vizuri nyama choma pamoja na mvinyo kidogo, utalala usingizi mzuri usiokuwa na ndoto za kuhuzunisha.
 
Ndoto , ukiziendekeza kila siku utakua na stress, kuna jamaa alihamia shule, ni kalokole kalifundishwa kwao eti kila ndoto ina maana hivyo niya kukemea, tukawa tunalala room moja, kako soft soft sanaaa, Alikua akiota ndoto mbaya ati anaamka analia, anapiga ukuta, shindwa shindwaa.

Hio siku nilimpiga mkwara, ole wako utupigie kelele tena, unatuletea uchuro humu.

Akawa akiamka analia ndani ya blanketi au anaenda kwenye korido,

Baadae akili zilimkaa sawa, mtu unaota umeokota gari, usiku huo huo linapotea, unaamka unalia, unasema kuna Kitu kibaya.

Rubish.
 
Ndoto huwa ni mawazo yanayojirudi kwa kile unachokifikiria.
Wakija watu wa imani hapa, watakutisha. Kwa ushauri wangu, leo kula vizuri nyama choma pamoja na mvinyo kidogo, utalala usingizi mzuri usiokuwa na ndoto za kuhuzunisha.
Ndoto ndio njia ya Mungu kuongea na watakatifu wake...

Ndoto ni njia ya Shetani kuongea na Mawakala wake...

Ndoto pia zipo za mawazo ya mtu
 
Acha kuchukulia maisha simple hivyo..hiyo tafrisiri ni wafanya midhaha..
 
Ndoto ndio njia ya Mungu kuongea na watakatifu wake...

Ndoto ni njia ya Shetani kuongea na Mawakala wake...

Ndoto pia zipo za mawazo ya mtu
Ni mtazamo wa watu wanaoishi kiimani, ila kama unaishi kisayansi, kunakuwa hakuna ukweli wowote, zaidi ya ubongo kucheua kile kilichopo katika mawwazo yako.
Ubongo wa binadamu una GB milioni 2.5, kuna wakati kichwa kinajaa, pale kinapokuwa kinacheua wakati wa utulivu ndio unapopata mawazo ya hapa na pale (ndoto).
Watu wa imani ambao hawataki kutumia sayansi kwenye kupata ukweli watasema, unalogwa mara kuna maono n.k​
 
It means loss of identity. Kwenye ulimwengu wa roho utambulisho wako umefutwa, umegawanywa na umetupwa. Sio ndoto nzuri inakufaa usali sana. Inaweza kuwa utambulisho wako kazini, kwenye ndoa/ mahusiano, nk ni vita hiyo lazima upambane, lakini sio ya mwili ni ya kiroho. Angalia maisha unayopitia sasa, kama kuna kitu umepoteza au unakaribia kupoteza jua ndio hicho. Unatahadharishwa kwamba hilo jambo limeanzia rohoni pambana ku reverse.

Habakuki 2:3
[3]Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
 
Acha kuchukulia maisha simple hivyo..hiyo tafrisiri ni wafanya midhaha..
Tatizo lako, wewe tayari ulishakuja na majibu yako; ni sawa na kwenda kwa daktari na kumwambia unaumwa malaria, badala ya daktari yeye ndio akuambie wewe ndio unaumwa malaria.​
 
Kufutwa na kiwembe kivipi mkuu ulishuhidia ikifutwa?Hebu tuanzia hapo umejuaje kiwembe ndio kimefuta?
 
It means loss of identity. Kwenye ulimwengu wa roho utambulisho wako umefutwa, umegawanywa na umetupwa. Sio ndoto nzuri inakufaa usali sana. Inaweza kuwa utambulisho wako kazini, kwenye ndoa/ mahusiano, nk ni vita hiyo lazima upambane, lakini sio ya mwili ni ya kiroho. Angalia maisha unayopitia sasa, kama kuna kitu umepoteza au unakaribia kupoteza jua ndio hicho. Unatahadharishwa kwamba hilo jambo limeanzia rohoni pambana ku reverse.

Habakuki 2:3
[3]Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Ooh!!Hii ni vita kweli..wachawi sio watu
 
Back
Top Bottom