kelao
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 8,132
- 5,800
Kifupi ni kuwa,nina biashara yangu yenye mtaji usiozidi milioni tatu (3000000/-)mwaka wa kodi nilikadiriwa kodi ya serikali ambayo nalipa awamu nne kwa mwaka.mpaka sasa nimeshalipa awamu 3 imebakia awamu moja ya tar.31 Dec. Kodi nyingine ambazo nimeshalipa mpaka sasa ni :kodi ya chumba cha biashara, leseni ya biashara, TFDA, ushuru wa uzoaji taka kila mwezi, kodi ya nyumba ninayoishi pango la miezi 6.sasa wamefika maofisa wa TRA wiki iliyopita na kusema wanakagua mashine za efd, niliwaambia sina uwezo kuinunua lakini waliniambia kosa kwa mujbu WA sheria. Nilijaribu kujieleza lakini hawakunielewa. Mwisho wakafunga biashara yangu na kunitaka niwe nayo ndani ya siku 7.kwa hakika nimeumia ndo maana nawauliza ndugu zangu hii iko sawa au ni uonevu you! CC:waziri wa fedha Dr Mpango