Jamani hili la TRA kufunga biashara yangu kwa kutokuwa na mashine ya efd's lipo sawa au ni uonevu uliopitiliza?

kelao

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
8,132
Reaction score
5,800
Kifupi ni kuwa,nina biashara yangu yenye mtaji usiozidi milioni tatu (3000000/-)mwaka wa kodi nilikadiriwa kodi ya serikali ambayo nalipa awamu nne kwa mwaka.mpaka sasa nimeshalipa awamu 3 imebakia awamu moja ya tar.31 Dec. Kodi nyingine ambazo nimeshalipa mpaka sasa ni :kodi ya chumba cha biashara, leseni ya biashara, TFDA, ushuru wa uzoaji taka kila mwezi, kodi ya nyumba ninayoishi pango la miezi 6.sasa wamefika maofisa wa TRA wiki iliyopita na kusema wanakagua mashine za efd, niliwaambia sina uwezo kuinunua lakini waliniambia kosa kwa mujbu WA sheria. Nilijaribu kujieleza lakini hawakunielewa. Mwisho wakafunga biashara yangu na kunitaka niwe nayo ndani ya siku 7.kwa hakika nimeumia ndo maana nawauliza ndugu zangu hii iko sawa au ni uonevu you! CC:waziri wa fedha Dr Mpango
 
Ondoa shaka.kanunue.ni laki mbili na nusu.alafu kawaonyeshe risiti.watakufungulia.
Ukipata mashine.
KAJIFUNZE JINSI YA KUITUMIA KWA WAFANYA BIASHARA WA KARIAKOO.
Mkuu wapi huko zinakouzwa laki mbili na nusu?
 
Kwa mwezi yanafika ml. 1150000/-kiongozi
1150000X12months = 13,800,000! Bado kidogo. Kuwa na mashine inatakiwa uwe na turn over ya kuanzia milioni 14 kwa mwaka. Huenda watakuwa wamekufanyia makadirio na kuona kuwa 'umeshahitimu'...
Tafuta tu hiyo hela ukanunue hiyo mashine kwa kuwa hata usipoinunua leo, kwa trend ya biashara yako itabidi uinunue ndani ya miezi miwili mitatu...
Kama huna pesa kwa sasa, mwandikie meneja wa TRA kwenye wilaya yako umuombe wakupe muda wa miezi mitatu uweze kukusanya pesa ya kununulia hiyo mashine.

Ondoa shaka.kanunue.ni laki mbili na nusu.alafu kawaonyeshe risiti.watakufungulia.
Ukipata mashine.
KAJIFUNZE JINSI YA KUITUMIA KWA WAFANYA BIASHARA WA KARIAKOO.
😀😀😀 Nimeipenda hii sentensi yako ya mwisho! Tena umeiandika kwa herufi kubwa. Naimani imebeba ujumbe mzito...
 
Nina shaka mtaji ulioutaja Tra hawezi kukwambia uwe na machine ya EFD kwa 3m mtaji nakataa ukiweka data za uongo zinapelekea kupata ushauri usiotatua tatizo lako, be true
 
Pole sana ila nao wamefanya ubinadamu kidogo maana kama wameona biashara yako inapaswa kuwa nayo ambayo inamapato sio mtaji zaidi ya Tshs 14m basi walitakiwa kukupiga fine ya Tshs 3m kiwango cha chini na Tshs 4.5m kiwango cha juu hayo ni matakwa ya sheria ya EFD. Kwahiyo katika makadirio kuna mahali ukuweka sawa ndio imetengeneza huo mwanya sasa kama hauko kwenye nafasi au uwezo wa kununua andika barua kwenye tawi husika ukiomba wakupe miezi mitatu utakuwa umefanya mambo yako vizuri au unaweza kuomba kupunguziwa makisio ya mapato ambayo yatakuwa chini ya 14m ili usiwe nayo kabisa.
Kila la heri
 
Nashukuru Mkuu kwa ushauri huu
 
Nina shaka mtaji ulioutaja Tra hawezi kukwambia uwe na machine ya EFD kwa 3m mtaji nakataa ukiweka data za uongo zinapelekea kupata ushauri usiotatua tatizo lako, be true
Huo ndo ukweli Mkuu, pamoja na kuwa sijafanya stock lakini haizidi 5ml.
 
Pole sana ila nao wamefanya ubinadamu kidogo maana kama wameona biashara yako inapaswa kuwa nayo ambayo inamapato sio mtaji zaidi ya Tshs 14m basi walitakiwa kukupiga fine ya Tshs 3m kiwango cha chini na Tshs 4.5m kiwango cha juu hayo ni matakwa ya sheria ya EFD. Kwahiyo katika makadirio kuna mahali ukuweka sawa ndio imetengeneza huo mwanya sasa kama hauko kwenye nafasi au uwezo wa kununua andika barua kwenye tawi husika ukiomba wakupe miezi mitatu utakuwa umefanya mambo yako vizuri au unaweza kuomba kupunguziwa makisio ya mapato ambayo yatakuwa chini ya 14m ili usiwe nayo kabisa.
Kila la heri
Asante mkuu, naufanyia kazi ushauri wako mara moja,nitakufa njaa mjini hapa
 
Ondoa shaka.kanunue.ni laki mbili na nusu.alafu kawaonyeshe risiti.watakufungulia.
Ukipata mashine.
KAJIFUNZE JINSI YA KUITUMIA KWA WAFANYA BIASHARA WA KARIAKOO.
zinapatikana wapi kwa laki mbili na nusu??
 
Ondoa shaka.kanunue.ni laki mbili na nusu.alafu kawaonyeshe risiti.watakufungulia.
Ukipata mashine.
KAJIFUNZE JINSI YA KUITUMIA KWA WAFANYA BIASHARA WA KARIAKOO.
Zinakouzwa 250,000 ni wapi?
Wadau wameikubali bei wanataka kujiweka sawa kuepuka mivutano na tra.
 
Back
Top Bottom