Jamani hili la TRA kufunga biashara yangu kwa kutokuwa na mashine ya efd's lipo sawa au ni uonevu uliopitiliza?

Mbona kuna meneja wa Tra wilaya fulani namfahamu ana biashara yake fulani lakini yeye hana mashine ya EFD au ndo mkuki kwa Nguruwe
 
ww ulipata mauzo yako yanafikia kiasi gani kwa mwaka?, au kodi unalipa kiasi gani kwa mwaka or kila installment ili tukusaidie kisheria zaidi
 
ww ulipata mauzo yako yanafikia kiasi gani kwa mwaka?, au kodi unalipa kiasi gani kwa mwaka or kila installment ili tukusaidie kisheria zaidi
Ukipiga kwa mwaka unapata ml. 13800000/-lakini ukweli ni kuwa huwezi kuwa kwenye biashara siku zote 365 za mwaka. Kodi niliyokadiriwa ni 318000/-kwa mwaka, mpaka sasa nadaiwa 79500/-awamu ya mwisho tar. 31 Dc.
 
Ondoa shaka.kanunue.ni laki mbili na nusu.alafu kawaonyeshe risiti.watakufungulia.
Ukipata mashine.
KAJIFUNZE JINSI YA KUITUMIA KWA WAFANYA BIASHARA WA KARIAKOO.
umedanganywa nanani?? mashine kwa dar nikuanzia 750,000 nakuendelea nawajua mawakala wote wanauza hizo mashine. Mim yangu nilinunua mwez july mwaka huu
 
Unafanya biashara gani na biashsra yako ipo eneo gani?? Tunanzie hapo kwanza kabla ya kulaumu na kulalamika
 
umedanganywa nanani?? mashine kwa dar nikuanzia 750,000 nakuendelea nawajua mawakala wote wanauza hizo mashine. Mim yangu nilinunua mwez july mwaka huu
USIBISHE KITU USICHOKIJUA.wewe sio mungu.nikikuletea hyo kampuni utatoa nini??
 
USIBISHE KITU USICHOKIJUA.wewe sio mungu.nikikuletea hyo kampuni utatoa nini??
Labda una njia nyingine. ila mwenyewe nlitafuta saana cheaper than that nkakosa, nkapelekwa kariakoo ambazo nlishauriwa nisichkue zitasumbua mbele ya safari. Cheapest ni 750k.
 
Hio kampuni uitoe wapi?? sio dagaa zile nikampuuni 11 tu ndo zilizo namamlaka yakusambaza mashine ya efd. Mashine ya Efd aina ya DATES DP5 ndio mashine cheap kabsa lakin hata huko sofia bulgaria ilikotengenezwa haiuzwi kwa 250k
 
wao wenyewe tra wanajua mambo magumu hivyo wanajaribu kulazimisha
 
Biashara ipo mkoani, ni duka larejaereja
Mkoani ndo mkoa gani?? Duka la rejareja ndo duka la bidhaa gani?? Nakuuuliza nikusaidie na nikushauri vyema unabakia kuficha ficha ila malalamiko yako umeweka wazi.

Ngoja nikusaidie tu kwa kifupi na uelewe kwann nimekuuliza maswali hayo.

Kama mtaji wako hajafikia kiwango ama threshold ya kutumia EFD mashine sheria baada ya kuboreshwa inawataka watu wanaofanya biashara maeneo ya mijini ambayo ni potential areas na ambayo pia hupangwa kutegemea na kodi zinazotozwa eneo hilo lakn pia biashara zote za huduma ni lazima kutumia EFD mashine.
 
Labda sijaeleweka tu mkuu, nipo iringa, duka la rejareja ni vitu mix, yaani kuna vyakula, vinywaji baridi na kali, viungo vya chakula, sabuni mafuta, na mahitaji yote ya nyumbani madogomadogo. Ila ni mjini kabisa
 
Hio kampuni uitoe wapi?? sio dagaa zile nikampuuni 11 tu ndo zilizo namamlaka yakusambaza mashine ya efd. Mashine ya Efd aina ya DATES DP5 ndio mashine cheap kabsa lakin hata huko sofia bulgaria ilikotengenezwa haiuzwi kwa 250k
Nimekuuliza.nikikitajia hyo kampuni utanipa nini??
 
Labda una njia nyingine. ila mwenyewe nlitafuta saana cheaper than that nkakosa, nkapelekwa kariakoo ambazo nlishauriwa nisichkue zitasumbua mbele ya safari. Cheapest ni 750k.
Nikikutajia hyo kampuni utanipa nini??
 
Kwa kuwa nyie wabishi.nawatajia jina la kampuni tu.
PERGAMON GROUP LIMITED.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…