ukifuata ushauri kama huu..ujue umepotea moja kwa moja na utachanganyikiwa utakapoinga kwenye ndoa.hebu tuchambue kidogo tuone madhara ya ushauri huu:
1. changudoa - huyu ni kiumbe yuko kazini - akili,mawazo na fikra yake haipo kwako na hujizuia kabisa kutokuwa emotionally involved na wewe mtakapokuwa wawili. Ataweza kukufanyia mambo ambayo mkeo hatakufanyia kamwe.sasa uzoefu kama huu utafanya nao nini ukishaoa? Huoni kila mara utataka urudi huko kupata ladha ambazo mkeo hatakupa?
2.shoga - huyu ni mwanaume mwenzio - kuanzia muonekano, haiba, feel of the body etc hafanani na mwanamke.uzoefu kama huu huoni hauna maana yoyote kwako ukiachilia mbali kuwa ni chukizo mbele ya mungu wako?
3.visichana under 18 - kwanza unabaka na unaweza kuishia jela miaka 30 na kuendelea na usije kuoa kabisa. Unatafuta nini hapa? Ukibahatika kutokuiona jela, huoni wewe utakuja kuwa hatari kwa jamii hata watoto wako mwenyewe endapo utafurahia visichana vidogo? Je hiki ndicho unachokitaka?
4. Mke wa mtu mwingine - na wa kwako je akijakuonjwa na mwanaume mwenzio mwenye mtizamo kama huu utajisikiaje?