Jamani hivi nini kazi ya akili?

Jamani hivi nini kazi ya akili?

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Kuna kazi nyingine sidhani kama wahusika zilizomo zimo! Ukishuka kwenye usafiri wa umma mbezi mwisho na ikatokea ukawa na kabegi, jinsi ambavyo unadakwa na wapiga debe sio poa! (si mwanaume si mwanamke)!

Daaah! Wengine wakiona gari la mbagara wanaanza kugombania abiria wakiwa ndani ya basi "yule wa kwangu aliyekaa siti ya nyuma"?

Utadhani walihaidiana kuwa naenda mikoani? Hivi kazi kama hii kweli unapata shilling ngapi? Akili zimeenda wapi?
 
Pesa inatafutwa kwa Tabu Mkuu, usishangae kuona watu wanakuvuta (Wanatafuta pesa).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Wewe unaevaa shati jeupe na Tai mwisho wa mwezi unapokea laaki nane na makato juu humfikii uyo anaingiza 40000 Kila sku isiyo na makato
 
Kukuchangamkia ndo kazi ya akili hiyo,au we ulidhani wafanye kazi gani ndo uwaone wana akili.
 
Vchwa 20 n ving kwa wingi wao pale stend ila iko hiv akipata abiria wa mwanza au dodoma yeye upata 5000 kama posho yao akikupeleka kwenye gar au ofisin wao uita chagora., kwaio kwa siku kuingiza 40000 n jambo la kawaida kabsa wapo wanaojielewa na wanafanya maisha na wapo wahun wao n kula na kulewa tu
Tuseme Kila kichwa anapewa buku 2, unataka useme kwa siku anakosa vichwa 20?
 
Wala usipate shida. Wakikusogelea tu waambie unaenda moro na una ticket ya Abood watakupotezea haraka sana. Abood hatoi posho.
 
Huyo ndo mwenye akili Sasa, siyo wewe akili ipo kwenye vyeti.
Kuna mtu alinipaga vyeti vyake vyote akaniambia kuwa makini hapo ndo maisha yenyewe, halafu huyo mtu kasoma masters, nilimshangaa sna.
Nikajiuliza Yule ambae hata hata cheti Cha kuzaliwa asemeje Sasa?
 
Nikiwa Raisi wa TZ hao wote watasombwa kwenye maroli wataenda kumwagwa mto Ruvu waliwe na mamba.
Kuwa na binadamu wanaoleta fujo ni bora ukahukumiwe na Muumba.
Wakina Hitler,Idd Amini bado tupo hawajaisha ila tu hatujapata mamlaka. Yakisomba maroli mawili tu wengine wakapata habari wenzao wanakopelekwa, wote watapotea stand yaani wataenda kutafuta kazi halali na stand zitakuwa safi na heshima.
 
Back
Top Bottom