Jamani huyu binti yangu ataniua kwa presha....

Jamani huyu binti yangu ataniua kwa presha....

karithi huyo fuatilieni utoto wenu wewe na mke wako

Sasa naona kibao kinatugeukia.......... Kwa mama watoto wangu naweza kukanusha moja kwa moja........... kwa kweli mke wangu hana hata chembe ya tabia hizo, ni mtulivu na sio muongeaji kihivyo. mara nyingi huji-keep low profile, na hapendi kujichanganya sana na watu......
Ni bahati mbaya nimepoteza wazazi wangu wote wawili, labda wao wangeweza kufumbua hiki kitendawili.......................
 
Kwanza alikuwa ni binti mtaratibu sana na hakupenda kuongea ongea, mara nyingi alikuwa akipenda kuangalia TV na video za katuni tu, haya mabadiliko na kibri vimeanza muda si mrefu, tuseme tangu aingie darasa la pili mwaka huu

...kibri?...pls be optimistic bana, sio kila mwanao atapoku challenge ana maanisha kibri...
anza kubadilisha mtazamo huo kwanza ndipo utapobaini jinsi gani waweza msaidia.
 
Mkaribishe humu JF tubadilishane mawazo naye, ashakua kiakili huyo.
 
Aise kaka kma mtoto basi huyu umezaa,maana si mchezo! Sijui dini yako ila kma ni mkristo biblia inaruhusu kuchapa watoto wetu,ila usichape tu bila kumwambia,mwambie kibuli kwa mama yake si kizuri akiendelea mchape,ila kwenye confidence mpe moyo aendelee ivyo ivyo, ila mfunze kuheshimu wazazi na mawazo ya watu wengine,sio kila siku yeye ndo atakua sahihi
 
Binti yangu ndio kwanza ametimiza miaka 7 mwaka huu, lakini amekuwa na mabadiliko makubwa sana kitabia. Ni mwaka huu ndio ameingia darasa la pili na amekuwa ni mdadisi na mbishi kupindukia.

Kuna wakati kama tunaangalia kipindi kwenye TV, naweza kutoa maoni yangu juu ya kipindi hicho, kama maelezo yangu hayatakuwa sahihi kulingana na uelewa wake, basi atabishana na mimi na mara nyingi anatoa reference za mwalimu wake (yaani jinsi walivyofundishwa) au kama aliwasikia wanafunzi wenzake wakilizungumzia jambo hilo, hata kama atakauwa amepotoshwa.


Nikiwa kama mzazi, najaribu kumuelewesha kulingana na umri wake lakini unaweza kuzuka ubishi mpaka nakereka. Mh! Watoto wa siku hizi wamekosa kweli adabu. Mfano, kulikuwa na tangazo la Kondom kwenye TV. Wakati tangazo likiendelea akaanza kusema, ‘hizi kondom ndio zinazotumika kuzuia maambukizi ya Ukimwi’

Mimi kwa hekima nikamuuliza kwamba, ni nani amemfundisha, akanijibu kuwa ni mwalimu wao. Nikamwambia ni kweli lakini sio ukimwi tu bali pia hutumika kwa uzazi wa mpango………..
Basi alinikata kalma na kuniambia kuwa uzazi wa mpango wanatumia vidonge vya majira na sindano za kuzuia mimba……………… He! Nilishikwa na butwaa. Mke wangu alinitupia jicho kali kama ananionya, ikabidi nikae kimya……….. nikajua nimechemsha.

Haikuishi hapo, siku iliyofuata alinijia na vipeperushi viwili, kimoja kinachoelezea njia mbalimbali za uzazi wa mpango na kingine kilikuwa kikielezea juu ya maambukizi ya Ukimwi, pamoja na kinga zake, na alikuwa anataka kuthibitisha kile alichokuwa akikisema siku iliyopita.

Nilijaribu kumuelewesha kwamba, mambo hayo sio wakati wake kujifunza kulingana na umri wake, nilimshauri asubiri akiwa mkubwa atajifunza mambo hayo kwa undani. Lakini alizidi kusisitiza kwamba anataka kunithibitishia kwamba jana alikuwa sahihi. Ilibidi nikubali kuwa alikuwa sahihi ili kuepuka malumbano.

Amekuwa na tabia ya kunikosoa bila hata ya aibu na si mimi tu hata mama yake pia hutofautiana naye kwa mambo madogo madogo. Anaweza kutumwa aandae meza kwa ajili ya chakula, yeye anachofanya ni kuondoa vitu vilivyopo mezani tu na kukaa kimya akiulizwa kwa nini hajaandaa meza, anadai ameshaandaa na ndio maana iko safi na haina kitu. Mama yake akimuuliza kwa nini hajaweka sahani na maji na vitu vingine. Anamwambia hakuwa specific, ‘ulitakiwa uniambie nitenge chakula’ atasema, akimkosoa mama yake.

Hebu nisaidieni nimfanyeje binti huyu…………………………?

mtoto anafundishwa uzazi wa mpango! dah dunia imeisha.yaani haja kimwili wala akili lkn tunachomeka plug kubwa kwenye tundu dogo.
 
malezi mabovu na kukosa adabu, ndo ubaya wa kuiga udhungu,hivi ungeku wewe enzi izo za baba yako ungefanya ivyo anavyo fanya mwanao?
 
Mbona madogo hayo? Nimeshuhudia! Sasa hivi mtoto wa darasa la saba anatumia vidonge vya uzazi wa mpango. Mimi nahisi huyo ticha anamnanilii kidogo kidogo. May be anamfundisha huyo dogo practicaly. Hapo umeumia. Mwamishe shule.
 
Mtambuzi, pole kwa yanayotokea hapo kwako. Kwa mawazo yangu. Ninaona umepata mtoto mwenye upeo wa tofauti kiakili. Akili alizonazo si za level yake ''genius''. Ingawa kuna masuala mazito ya kitaalamu sana yanaweza pia kuwa sababu.
 
Mtambuzi,wala usifikie mawazo mabaya ya kumchapa hata kidogo isipokua la msingi mueleze kuheshimu wakubwa hasa nyie wazazi wake pindi mjadilipo jambo lakn wakati huohuo ni vema ukaelewa huyo mwanao ana akili sana maana kuna watoto wengine umri kama huo lakn ukiwa kama mzazi unahisi kwamba hapa hakuna kitu ila zaidi kama wewe ni mkristo au muislam jitahidi awe anapata muda wa kwenda kwenye mafundisho ya dini baada ya kutoka shule,nina uhakika ana uwezo mkubwa huyo mwanao wa kuelewa mambo
 
Back
Top Bottom