Hapo ndio penye tatizo, huenda wewe hukupata mafundisho vizuri ya ndoa au umepata ila ulijisahau. Mwanamke anapokuwa mjamzito (sio wote) kuna baadhi ya tabia hubadilika, anaweza kuwa mkali, akamchukia mtu hata wewe mwenyewe, akapenda sana vitu fulani ambavyo hakuwa anavipenda before, anaweza akawa ananuna nuna mara kwa mara inategemea mimba imempelekaje. So wewe ndio unatakiwa uwe faraja kwake na ujue hiyo hali ni kwa ajili ya mimba tu na si vinginevyo. Sasa unapaswa pia kuvuta subira mara baada ya kujifungua maana hiyo hali haiishi mara moja tu baada ya kujifungua, inachukua muda kidogo (pia hutegemea na mtu na mtu)<br />
<br />
Kwa hiyo nakushauri mvumilie tu itaisha tu baada ya muda fulani hasa kama hakuwa hivyo mwanzo, pia muonyeshe upendo zaidi kipindi hiki alichojifungua huenda pia wewe hauko karibu naye kwa sababu yeye yuko busy na mtoto, jichunguze na wewe pia