Jamani huyu rita kumbe ni mswahili?

Jamani huyu rita kumbe ni mswahili?

Simba Mkali

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
620
Reaction score
239
DEMU anasoma chuo cha Mipango pale Dom, ni mwenyeji wa Mbeya mwenye maskini Pwani alitongozwa na jamaa mmoja wa mjini, jamaa alikuwa na mipango mingi na huyo nyapu, kumbe Rita wala hakuwa na habari na jamaa, wakakaa na kunywa na kuongea mambo mengi kuhusu maisha, mshikaji akasema amepata mtu mzuri wa kupanga naye maisha... loh Kumbe Rita wala hana mipango na jamaa,akasema kesho yake anaanza mitihani, wakaachana jamaa akarudi mjini.

Kukawa na mawasiliano kati yao siku nyingine jamaa akatimba Dom si akawasiliana na Rita wake, akahakikishiwa kuwa watakutana, kila akipiga simu anaambiwa subiri, subiri mwishowe ikawa shubiri, usiku Rita hakuwa akipokea cm tena alikuwa akila starehe na Mbunge mmoja mtu mzima. Jamaa alipokuja kupeleleza akajuta kwanini alimfahamu Rita, mpaka leo hii analalamika kwa kupotezewa muda na Rita, tena anasema Jamani huyu Rita ni mswahili anadai kuwa kwanini asingechomolea tangu siku ya kwanza?
 
teh teh teh, chezeya wadada wa vyuo ww, pole yake rafikiyo,
Rita wake anakamua posho ya muheshimiwa,
 
bunge likiwa on session! huwa hawapatikani wadada wengi wa dom! chezeiya hawara yake ya lulu n co! pole yake huyo mtu!
 
kwa nini neno 'uswahili' linatumika kama sifa mbaya? je ni watu hatuupendi utaifa wetu au nini hasa?
 
Ali kayuti muandikaji mzuri wa script!
 
Ali kayuti muandikaji mzuri wa script!
Siyo Ali Kayuti.... Mkuu ni Ali Yakuti siyo mwandishi wa script ni mwizi wa script anayekwenda kumuuzia Ray. Hata hivyo hii siyo script ni kisa cha kweli kabisa.
 
DEMU anasoma chuo cha Mipango pale Dom, ni mwenyeji wa Mbeya mwenye maskini Pwani alitongozwa na jamaa mmoja wa mjini, jamaa alikuwa na mipango mingi na huyo nyapu, kumbe Rita wala hakuwa na habari na jamaa, wakakaa na kunywa na kuongea mambo mengi kuhusu maisha, mshikaji akasema amepata mtu mzuri wa kupanga naye maisha... loh Kumbe Rita wala hana mipango na jamaa,akasema kesho yake anaanza mitihani, wakaachana jamaa akarudi mjini.

Kukawa na mawasiliano kati yao siku nyingine jamaa akatimba Dom si akawasiliana na Rita wake, akahakikishiwa kuwa watakutana, kila akipiga simu anaambiwa subiri, subiri mwishowe ikawa shubiri, usiku Rita hakuwa akipokea cm tena alikuwa akila starehe na Mbunge mmoja mtu mzima. Jamaa alipokuja kupeleleza akajuta kwanini alimfahamu Rita, mpaka leo hii analalamika kwa kupotezewa muda na Rita, tena anasema Jamani huyu Rita ni mswahili anadai kuwa kwanini asingechomolea tangu siku ya kwanza?
Pole best najua yaliyomkuta haya ni wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom