Kabla ya kuugua uvimbe tumboni,akiwa na mkewe Wastara ambaye pia alikatika mguu katika ajali ya pikipiki walioipata.
Pichani juu: Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki' (mwenye miwani) akiwa katika sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen iliyofanyika Aprili 15, mwaka huu.
Stori: Gladness Mallya
UKWELI ni kwamba, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki' anaumwa, Ijumaa limemshuhudia na linakuhabarisha.
Hali ya Sajuki imeendelea kuwa mbaya akidhoofu mwili siku hadi siku kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa.
Aprili 15, mwaka huu Sajuki na mkewe Wastara Juma walifanya sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen ambayo ilihudhuriwa na waandishi wetu waliomshuhudia msanii huyo akiwa amedhoofu sana.
WASANII WAMTOLEA MACHOZI
Kabla ya kuugua, Sajuki alikuwa mwanaume aliyeshiba (mnene) na mwenye nguvu hivyo kutokana na hali yake ilivyobadilika na mwili kuwa mdogo, baadhi ya wasanii waliofika kwenye sherehe hiyo walijikuta wakimtolea machozi.
"Jamani tuacheni utani, Sajuki anaumwa sana na anahitaji msaada na maombi yetu ili arejee kwenye hali yake ya kawaida," alisema mmoja wa waigizaji wenzake.
SAJUKI KURUDI INDIA
Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
WADAU TUMSAIDIENI SAJUKI
Kufuatia hali ilivyo, gazeti hili linaomba wadau tujitokeze kumchangia Sajuki fedha kwa ajili ya matibabu kupitia simu ya mkononi kwa kutuma kwenye Tigo Pesa namba 0713 666 113 au kwenye akaunti namba 050000003047 katika Benki ya Akiba Commercial yenye jina la Wastara Juma Issa.
Hawa ni waigizaji katika tasnia ya maigizo na filamu hapa nchini.Walikutana katika filamu ya mboni yangu na kuwa wapenzi.Katika mapenzi yao walivalishana pete za uchumba na hatimae kupanga kufunga ndoa.Siku chache kabla ya ndoa yao walipata ajali na Wastara kuvunjika kabisa mguu.
Watu wakajiuliza kweli Sajuki atamuoa Wastara pamoja na kukatwa kabisa mguu?Baada ya wastara kupona jeraha ndoa yao ikafungwa dada akitembea kwa magongo.Baadae alifanikiwa kupata mguu wa bandia na sasa anatembelea mguu wa bandia.
Mitihani haikuishia hapo katika familia hii ambayo wamejaaliwa mtoto mwenye mwezi mmoja na siku kadhaa.Sasa hivi Sajuki anaumwa sana maradhi ambayo yalifanya mpaka apelekwe India kwa matibabu.Inasemekana ana uvimbe tumboni,alipopelekwa India ilishindikana kufanyiwa matibabu maana Sajui alikuwa dhoofu sana.Akarudishwa Tanzania ili afanye matibabu na kurudisha angalau nguvu kidogo ya kwenda kuanza matibabu ya huko India.Miezi miwili ijayo atalazimika kusafiri kwa ajili hiyo.Watanzania wameombwa kushirikiana na familia hii kufanikisha hili ikiwemo michango ya pesa.
Nimefikiria huyu ni mwanamke tena bado binti lakini yupo na wakati mgumu sana wa kuuguza huyu mume. Inasemekana Wastara ni yatima mumewe ndio roho yake. Hivyo nikachukua shauri la kumuita kesho kwenye leo tena tuzungumze atupe picha kamili watanzania na tuone tunamsaidiaje katika mtihani huu.Anasema ameshalia sanaaa katika maisha yake maana kila kukicha anapata mitihani.Mitihani tumeumbiwa binadamu lakini je tunasaidiana vipi katika hiyo mitihani?
Kwa msaada wa Dina Marios na Global Pulibshers