Jamani, jamani! Usiombe ukutane na hawa watu!

Jamani, jamani! Usiombe ukutane na hawa watu!

Wao wanaweza kuongea lakini sio fact wanaongea ili mradi dawa Yao ni kukaa kimya na kutojibishana nao
 
Ni watu fulani hivi, wajuaji lakini hawajui kama hawajui. Yaani hawajasoma ila wanajua kila kitu!

Hawa watu kama ndugu, jamaa, rafiki au majirani zako basi jiandae kisaikolojia. Utakuta hawana hela lakini ni kama wanazo vile. Hawana elimu kubwa ila sasa, kwa ujuaji huwawezi na wanajiamini sana!

Kila jibu wanalo hata kama sio sahihi. Hawa watu usiombee kuwafahamu
Unataka kila usemalo wakukubalie hata kama ni utumbo wamekukomesha
 
Wengi wao ni wabeba mikoba aka chawa. Kuna mambo ili uyafanikishe inabidi ukutane nao. Ila sasa, usipokuwa makini utajiona wewe ndio hujui. Wapo wengi. Wana msimamo kwelikweli na wanaamini bila wao hakuna kinachoweza kufanyika.
Dawa yao hoja kama huna uwezo wa kuwabana kwa hoja utaishia kuwalaumu
 
Halafu wanakuaga wabishi sana...
mimi kuna jamaa alikua anasema jamaica(jamdam) ipo africa,halafu ndio inaongoza kwa umasikini...
Ile nataka nimweleweshe ukazuka mzozo akafikia mpaka kuniambia elimu yangu nimesoma bure tu...
Hivi Tanzania ipo nchi Gani[emoji23][emoji23]
 
Halafu mbaya zaidi ukute ni vile vijitu vifupi vyenye miili minene yaani vituruma[emoji23][emoji23]
 
Unataka kila usemalo wakukubalie hata kama ni utumbo wamekukomesha
Kuna mmoja aliniambia fisi ana jinsia zote mbili so hakuna fisi dume Wala jike na wakijamiiana wanachomekeana wote ila atakayewahi kupizz ndio anambebesha mwenzake mimba[emoji23][emoji23][emoji23] halafu mbishie sasa uone moto wake
 
Ni watu fulani hivi, wajuaji lakini hawajui kama hawajui. Yaani hawajasoma ila wanajua kila kitu!

Hawa watu kama ndugu, jamaa, rafiki au majirani zako basi jiandae kisaikolojia. Utakuta hawana hela lakini ni kama wanazo vile. Hawana elimu kubwa ila sasa, kwa ujuaji huwawezi na wanajiamini sana!

Kila jibu wanalo hata kama sio sahihi. Hawa watu usiombee kuwafahamu
Hueleweki ujue, au ndo wewe?
 
Na hiyo ndio maana halisi ya mjuaji, mtu anayedhani anajua ila hajui au mtu anayebishana ilihali hayuko sahihi, sasa cha ajabu kuna wabongo hata mtu ambaye kweli anajua, au mtu ambaye anabishana na yuko sahihi eti naye wanamuita mjuaji, kumbe uhalisia ni kwamba wao ndio hawana hoja
 
Uwezi kuwa unajua kila kitu
Yani wewe kila kitu umo, siasa, uchumi, michezo, dini, mapenzi n.k kuna namna lazima utakua haupo sawa
Mkuu siyo dhambi kuwa jack of all trades hata kama ni master of none kuna watu wanapenda tu kufuatilia kila kitu
 
Mkuu siyo dhambi kuwa jack of all trades hata kama ni master of none kuna watu wanapenda tu kufuatilia kila kitu
Kufuatilia sawa ila kwenye kuona kuwa unajua kila kitu kushinda hata wenye kada hiyo sio. Mfano mtu anabisha suala la kitaalam kabisa wakati hana utaalamu wowote na hajabobea kwenye kada husika.
 
Walikuzidi kuongea? Au huwapedi?.
Hawa watu usipokuwa makini watakuambukiza ujinga. Yaani ni vigumu kuwatambua hadi uwe makini sana! Na ukikubaliana nao hawakawii kukusaliti.
Ni wepesi kubadili maana. Utasikia "mimi sikumaanisha hivyo, nilimaanisha hivi...." Hapo ujue anaanza kutengeza hoja nyingine tofauti na awali,
 
Back
Top Bottom