Pole Bishanga, siku hizi hakuna mtoto wa kike na wa kiume, wote wamekuwa pasua kichwa, naongea hivyo vile nawaona wadogo zangu wawili walionifuata wanavyomsumbua mama angu, anasema mpaka anaishiwa nguvu, fujo zao, club yao, pombe zao, wanawake wakubwa kwa wadogo wote wao, hawasikii la muazin wala la mnadi swala! Wakitoka nyumbani sa moja jioni bila kufika sa8 au 9 usiku hawajarudi nyumbani, huezi amini anaenifuata mgongoni ana watoto wawili kwa wanawake wawili tofauti tena wana umri sawa na dadangu wa kwanza, na wote katupiwa mama analea.....
Mama alishajichokea kuongea, siku hizi amebaki kulia na Mungu kwamba mbona anasali sana watoto wake wabadilike lakini hawabadiliki.... Endelea kumwombea binti, atabadilika, usikate tamaa bado mapema sana!