Jamani kulea mabinti ni kazi, kha!

Mwosha?
 
Hii thread natamani niidelete maana comments kama hizi zinatia uchungu sana.
 
Hana uwezo hata wa kujilisha mwenyewe huyo Kagame wacha wengine. Asituletee kufuru zake.

Siku ambayo rizki yako inafungwa hata uwe na mali vipi na hata ushindiliwe kwa mipira, haipiti.
 
Babu DC maneno mazito haya ingawaje yana ukweli ndani yake, angalia Bishanga asijejinyonga kwa hasira...
 
Huu ulimwengu wa sasa kwa kweli hakuna heri!
Kuweni karibu na watoto ie get involved in their day to day life!
Pia mjitaidi kuwaweka karibu na mola madogo ili nae awanyoshe!
 
wa kwangu sasa hivi natamani nimtafune nimmeze,presha imepanda,kichwa kinaniuma,yaani nasikia kizunguzungu,wana nini watoto hawa? Niacheni nilale nisije nikampasua kichwa!

Tabia hufuata mkondo. Check ur history pls!
 
Hahahaaa ni mimi kaka ila sikumaanisha.

Kamwe siwezi kabisa kufanya hivyo. Changamoto zozote zile aziletazo mimi nazichukulia kama baraka na wajibu.

Hapa sasa walau umeniaminisha kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya kufurahisha baraza!!

Hata mie huwa namweleza Bibi DC kuwa hiyo (blue) ndiyo raha yenyewe ambayo mtu ambaye hakubarikiwa kupata watoto anaikosa.

Ndo maana sijamwelewa mdogo wangu wangu Bishanga kwa nini analia lia!!
Hata jina lake amelikana mwenyewe...Hafai tena kuitwa Bishanga bashaija!!

Babu DC!!
 
Babu DC maneno mazito haya ingawaje yana ukweli ndani yake, angalia Bishanga asijejinyonga kwa hasira...

Hujambo SL?

Sasa wote tukikimbilia kumpa pole Bishanga, nani atamkumbusha yale alikuwa anawafanyia watoto wa wenzie??

Nimeonelea kwamba leo nijaribu kumkubusha kuwa hayo anayoyaona ni dibaji tu....Kitabu chenyewe bado kuona!!


Tabia hufuata mkondo. Check ur history pls!

Duuuuu,

Walau wewe umetuunga mkono kumkumbusha Bishanga kwamba mkuki kwa nguruwe.....!!

Naona ameshasahau kwamba hata vile vibinti alivyokuwa anakimbizana navyo na kuzeesha chakula ya watoto vina baba ba mama pia!!

Nadhani tumsaidie akubali tu kwamba hana uwezo wowote wa kubadilisha fate...

Amwombe tu Mungu amsaidie katoto kake kavuke salama!!

Babu DC!!
 
Hujambo SL?

Sasa wote tukikimbilia kumpa pole Bishanga, nani atamkumbusha yale alikuwa anawafanyia watoto wa wenzie??

Nimeonelea kwamba leo nijaribu kumkubusha kuwa hayo anayoyaona ni dibaji tu....Kitabu chenyewe bado kuona!!
Daah babu DC mie ndio mana ukipotea huwa nakumiss sana nimekugongea like kimoyo moyo,


maneno ya ukweli sana, ngumu kumeza ila Bishanga ajitahidi kusukumia hata na maji... Amesahau kuwa goes around comes around, wahindi huwa wanaita Karma, ukitenda mema utalipwa mema na ukitenda mabaya utalipwa mabaya, lini, wapi na kwa style ipi nobody knows! Nakubaliana na wewe babu DC kuwa Bishanga hana budi kuvumilia kipindi hiki kigumu kwake mpaka pale kitakapopita, hana cha kufanya zaidi sana amrudie Mungu wake na aungame makosa yake na asisahau kufanya maombi kwaajili ya binti!

Mie sijambo kabisa, nifikishie salamu kwa bibi mpendwa!
 

Ahsante SL,

Salamu zimefika na hayo pia nitamweleza (Blue).. Bahati nzuri Bibi DC anawapenda wajukuu wote kwa sababu ana imani na Babu .....Hafanyi uchakachuaji wa aina yoyote!!!

Bishanga atulie tu na kuona mafuriko haya (kama yale ya Jangwani) yataishia wapi!!

Akifanya mchezo anaondoka na maji nasi tunakula pilau (Mungu apishie mbali ...ingawa ni moja ya majanga yanayoweza kumkutua mdogo wangu)!!

Mbombo ngafu.....

Babu DC!!
 

Off topic,
Hivi Mkonge hotel bado ipo?

Leo nimeikumbuka sana hii hoteli.
 
Hahaha! Nadhani anatafakari ndio mana kapotea ghafla leo na sio kawaida yake, kweli yuko kwenye wakati mgumu sana, atulie tu hana jinsi! Tunamwombea kikombe kimuepuke mapema iwezekanavyo.....

Mwambie bibi wajukuu tunampenda sana pia na ajitahidi siku moja aje kutusalimu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…