Ndugu yangu Bishanga kulea hakuna formula wala kuwa mchungaji sio kwamba uchungaji wako ndo unalea watoto hapana,kuwa mchungaji na kumlea mtoto katika maadili ni vitu viwili tofauti,tuangalie watoto wanajifunza nini wakiwa wadogo kama kuna kitu anakifanya akiwa mdogo na hukipendi na hukuchukua hatua stahiki angali mdogo ujue akikua huwezi kirekebisha.Mfano mtoto anaweza akawa mdogo mzazi unamtuma kitu anakuambia sitaki na wewe unainuka kwenda kukichukua unadhani akikua atakutii?kwa mfano una mtoto wa kike na nyumbani una house girl kila kitu anafanya house girl huyo binti yako hutaki ajifunze hata kuosha vyombo unadhani akikua ataweza kufanya hivyo vitu kama hakujifunza akiwa mdogo?hapo hata kwa mume wake atakuwa mzigo,mume anataka ugali mke anasema mi sijui kupika ugali njoo upike mwenyewe,sio anafanya makusudi ni kweli hajui maana hakufundishwa huo ni mfano mdogo sana lakini nataka kukuambia tu mara nyingi mtoto analelewa na mazingira ya nyumbani kwao kama wazazi hawana muda wa kumfundisha atafundishwa na anaocheza nao au atafundishwa na TV kwa enzi hizi tulizonazo,nitakupa mfano hai mimi ni mtoto wa kiume lakini katika utoto wangu wazazi walinifundisha kuheshimu kila mtu mkubwa kwa mdogo tajiri kwa maskini bila kubagua,pia walinifundisha kujitegemea kwa mfano kufua nguo zangu mwenyewe,kuosha vyombo,kupika na hata kufanya usafi wa nyumba,hayo yote tuliyafanya kwa zamu maana watoto wa kiume tulikuwa lukuki katika familia baada ya kukua na kuanza kujitegemea ndo nikaanza kujua kile wazazi walichonifundisha kilikuwa na umuhimu gani ilihali wakati wa utoto niliona kama adhabu hivi.Kwa hiyo kuwa mzee wa kanisa,nabii,askofu,sheikh haimsaidii mtoto kuwa na tabia nzuri hiyo karama uliyonayo unatakiwa kuitumia sasa kulea mtoto hapo ndo atakuwa na maadili mazuri lakini sio kwa kuwa wewe mchungaji Mungu akufundishie watoto kuwa na tabia njema.Makundi pia anayokuwa nayo mwanao yana ushawishi mkubwa sana kaitka kujenga tabia ya mwanao,chunga sana aina ya marafiki wa mwanao