Media kama azam zinapaswa kutokuwa na upendeleo wa kuripoti matukio yote ya wananchi kwa usawa bila kujali itikadi za kisiasa, kikanda na kidini. Kama azam anafanya biashara na bidhaa zake anauzia kwa wananchi bila kujali ni wa itikadi gani za kidini, kisiasa na kikanda hata habari anatakiwa afanye hivyohivyo na sio kuona ukakasi na kinyaa kutangaza habari za siasa na dini zisizompendeza mmiliki. Leo ni ijumaa kuu azam inatakiwa ifanye coverage ya ibada hiyo makanisani wananchi wa imani hiyo waone hata kama mmiliki si mkristo ajue anatumia masafa ya umma na media yake si ya kidini kama tv imaan ambayo haiwezi kurusha maudhui ya kikristo