Jamani lugha yetu wenyewe, tuvalishwe vibao!!

Jamani lugha yetu wenyewe, tuvalishwe vibao!!

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,819
Reaction score
801
Wakuu, mimi nina utata kuhusu lugha yetu, mnisaidie mantiki yake. Kuna taratibu mbalimbali ktk shule mbalimbali hapa nchini ambapo mwanafunzi analazimika koutumia lugha ya kiingereza hata kama kwa shida. Asiye ongea kiingereza na akaongea kiswahili atavishwa kengele au kijibao chenye maneno ya maudhi kama " Shame you", " I am stupid by talking swahili" JAMANI lugha yetu wenyewe tunajipa adhabu!!!! kuna shule fulani mwanafunzi akiongea kiswahili anakula bakola si mchezo, jee hii ni sahihi?
 
Ni utaratibu tuliojiwekea baada ya kugundua kuwa watoto hawapendi kiingereza. Ndiyo, kiinglishi siyo lugha yetu lakini hatuna jinsi. Maana bila kujua lugha hii hasa wakati huu wa utandawazi imekula kwako. Heri tuvalishane vibao watoto wetu waijue lugha hii ili waweze kupambana kwa stahiki katika soko la ajira la dunia ya sasa. Ni ushauri na mtazamo tu.
 
Back
Top Bottom